• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TOVUTI za hospitali zitangaze mambo mazuri yanayofanywa na hospitali nchini

Tarehe ya kuwekwa: September 30th, 2019

MKURUGENZI wa TEHAMA wa Wizara ya Afya Haji Bamsi ameshauri kutumia tovuti za hospitali zilizoanzishwa kutangaza kazi kubwa ya kuokoa maisha inayofanywa na hospitali.

Bamsi alikuwa anazungumza katika mafunzo ya siku tano ya utengenezaji wa tovuti za hospitali kwa maafisa TEHAMA wa hospitali za rufaa za mikoa na hospitali tano za Halmashauri za wilaya yaliyofanyika mjini Morogoro.

Amesema kuna mambo mengi ambayo yanafanyika katika vituo vya kutolea huduma za afya lakini hayapati nafasi ya kutangazwa katika vyombo vya habari.

Amesema vyombo vingi vya habari vimekuwa vinatangaza habari mbaya zaidi zinazotokea katika vituo vya kutolea huduma za afya na kuacha habari nzuri zinaweza kuleta matokeo makubwa kwa wananchi

“Tovuti hizi za hospitali zisaidie kutangaza mambo mazuri mengi yanayofanywa na hospitali ili yaweze kufahamika kwa wananchi ikiwemo kutoa elimu kwa umma katika masuala mbalimbali ya afya’’,alisema.

Bamsi amesema kuna habari nyingi ambazo zinaendelea katika hospitali ikiwemo miradi mbalimbali ya afya,elimu ya magonjwa mbalimbali,kuelimisha kuhusu Bima ya Afya na CHF iliyoboreshwa ambazo hazipati nafasi ya kutangazwa katika vyombo vya habari.

Amesema tovuti zilizoanzishwa zikitumika vizuri zitasaidia wananchi wengi kupata taarifa nyingi za afya ambazo pia zinaweza kusambazwa katika mitandao ya kihabari kutoka katika tovuti na kuwafikia wananchi wengi.

“Hatutaki kusubiri kutangaza habari  za hospitali kwa matukio mfano kuzaliwa watoto hadi siku za sikukuu ndiyo zinatangazwa,wakati hopsitali zinafanyakazi kubwa ya kuzalisha watoto na kuokoa maisha ya watu kila siku’’,anasisitiza.

Mafunzo ya utengenezaji tovuti za hospitali yameratibiwa na TAMISEMI na  kuwashirikisha maafisa TEHAMA 65 kutoka katika hospitali za Rufaa za mikoa 28 na maafisa TEHAMA watano kutoka katika hospitali tano za Halmashauri nchini.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Serikalini

Septemba 30,2019

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa