Mkurugenzi manispaa ya Songea Tina Sekambo amewaasa Maaafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata,waandishi wasaidizi na BVR Kit Operators kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa, kwa bidi, na moyo wa kujituma katika kufanikisha zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili.
Hayo yametolewa leo na Mkurugenzi Manispaa ya Songea Tina Sekambo ambaye aliwakilishwa na Afisa Mazingira manispaa ya Songea Philipo Beno, katika Hotuba yake iliyosomwa ya ufunguzi wa mafunzo hayo ya waandikishaji wasaidizi, na BVR Kit Operator yaliyofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Songea leo 30/04/020.
aKIitoa wito kwa washiriki hao wa mafunzo kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na Tume ili waweze kufanyia kazi wakati wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari kudumu la Wapiga kura. Alisema “ zoezi hili la uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura awamu ya pili litafanyika kwa siku tatu kuanzia 02.05- 04.05.2020”
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Tume ya Taifa ya Uchaguzi Adam Mkina alisema” Mpiga kura anaweza kuhakiki taarifa zake kupitia simu ya kiganjani kwa kupiga namba *152*00# na kufuata maelekezo yatakayomwezesha kuhakiki taarifa zake au kupitia Tovuti ya Tume www.nec.go.tz kwa kubonyeza sehemu iliyoandikwa ‘Uhakiki’ na kuendelea kufuata maelekezo.”
Aliongeza kuwa Uwekaji wazi wa Daftari la Wapiga kura utazingatia tahadhari zote za Afya kuhusu kuzuwia maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virus vya CORONA.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY,
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa