Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Songea Mjini Tina Sekambo amefanya uteuzi wa majina ya wagombea Ubunge leo 25/08/2020 saa 10:00 jioni ambapo kati ya Wagombea Ubunge 8 waliochukua fomu za Ugombea Ubunge ni Wagombea sita “6” tu ambao wamerudisha fomu.
Wagombea nafasi ya Ubunge Songea Mjini ambao wamerudisha fomu za Uteuzi ni Damas Daniel Ndumbaro (CCM), Anna Daniel Kapinga (ADA TADEA), Aden Bahati Mayala (CHADEMA), khalifa Musa Tengeneza (NCCR-MAGEUZI), Likapo Bakari Likapo (ACT-WAZALENDO), Mambo Ahamadi Aroni (CUF).
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa