Ofisi ya Rais – TAMISEMI imetoa mafunzo ya Mfumo wa uratibu wa madai na madeni ya Watumishi – MADENIMIS kwa wataalamu wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kuwawezesha kupata uelewa wamatumizi ya Mfumo wa kuratibu madeni au madai kwa watumishi wa umma.
Mwezeshaji wa kitaifa Zezema Shilungushela alisema Mafunzo haya yametolewa kwa kwa wataalamu mbalimbali wakiwemo na Maafisa Elimu Msingi na Sekondari, Mweka hazina, Afisa takwimu Msingi na Sekondari, Afisa Utumishi, pamoja na Afisa TEHAMA, ambayo yalifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea 03-04/09/2020.
Alisema “Lengo la Mfumo huu ni kumwezesha mtumishi Kuanzisha dai lake kuona hatua zote za dai hilo linavyofanyiwa kazi katika ngazi mbalimbali pamoja na mambo mengine, Mfumo huu utasaidia Serikali kuwa na takwimu sahihi za Watumishi wenye madai/madeni na kiasi cha madai/madeni kinachodaiwa na Watumishi hao.”
Alibainisha kuwa Mfumo huu unajulikana kwa jina la MadeniMIS ambao unaratibu madai na madeni yote ya watumishi yasiyo ya mishahara (Non-Salary debits), na kwasasa mfumo huu unafanya kazi kwa Watumishi wa kada ya Ualimu katika Sekta ya msingi na sekondari.
Aliongeza kuwa hapo awali madai/madeni yalikuwa yanahakikiwa kwa njia ya kawaida na sasa yataratibiwa kwa kutumia Mfumo wa kieletronik.
Hata hivyo baada ya mafunzo hayo kutolewa, kuanzia leo 9-10/09/2020 Wataalamu hao wanaendelea na ufundishaji kwa waratibu Elimu kata, wakuu wa shule Msingi na Sekondari kwa lengo la kuwawezesha kufahamu jinsi ya kuutumia mfumo wa kuratibu MadeniMIS ndani ya Manispaa ya Songea.
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa