MADHUMUNI YA MKATABA
Dhumuni kuu la Mkataba wa Huduma kwa Mteja (Client’s Service Charter) ni kuongeza ufanisi na uwajibikaji, kuongeza ufahamu kuhusu aina ya huduma, ubora na upatikanaji wa huduma zitolewazo na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea. Mkataba unatoa ahadi kwako mteja juu ya:
MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
1.1 DIRA NA DHIMA
Halmashauri ya Manispaa ya Songea na wananchi wenye maisha bora na endelevu.
1.2 DHAMIRA
Halmashauri ya Manispaa ya Songea na wadau wa ndani na nje imedhamiria kutoa huduma bora na endelevu kwa Wananchi wake kwa kutumia rasilimali zilizopo na zitakazopatikana kwa kuzingatia vipaumbele vilivyowekwa kwa kushirikisha wananchi kwa njia za uwazi na za kidemokrasia ili hatimaye waweze kuinua kiwango cha ubora wa maisha yao ifikapo mwaka 2025.
2.0 LENGO KUU LA MKATABA
Lengo kuu la mkataba huu ni kuwepo kwa ubora wa huduma zinazotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Mkataba huu unafahamisha wadau wetu tuliyojipangia kufanya, jinsi ya kuwasiliana nasi, nini cha kutegemewa kuhusiana na huduma zetu, na jinsi ya kutoa maoni na malalamiko yao kuhusu huduma zinazotolewa. Mkataba pia utawezesha kushirikisha wadau katika kuongoza Halmashauri, utaonyesha mwelekeo wa wateja wetu, jinsi ya kudai haki zao katika Halmashauri yetu na pia utaonyesha uwazi katika kuwasiliana, kulalamika na upatikanaji wetu.
3.0 HUDUMA ZA OFISI YA MKURUGENZI WA MANISPAA
Miongoni mwa huduma zitolewazo katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea ni pamoja na kuwajengea uwezo wa kitaaluma watumishi wa Halmashauri ili waweze kutoa huduma bora, kupokea na kushughulikia malalamiko ya wananchi na maombi mbalimbali.
3.1 HUDUMA ZA JUMLA ZITOLEWAZO NA OFISI YA MKURUGENZI WA MANISPAA NI KAMA ZIFUATAZO:-
Halmashauri ya Manispaa ya Songea pamoja namajukumu ya kiutawala inatoa huduma mbalimbali kwa wadau wake kama ifuatavyo:-
Kuajiri, kuthibitisha kazini watumishi, kupandisha vyeo watumishi na kushughulikia maombi ya uhamisho wa watumishi na kuratibu utoaji wa huduma;
Kuratibu masuala ya utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa;
Kukusanya mapato na kufanya malipo ya huduma na bidhaa;
Kuendeleza na kuboresha mipango miji, maendeleo ya ardhi, kilimo na mifugo mjini, maliasili na mazingira;
Kusimamia ujenzi wa miundombinu ya barabara, majengo, umeme na maji;
Kuboresha maendeleo ya jamii, ustawi wa jamii na ushirika;
Kuratibu uibuaji wa miradi, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo;
Kutoa huduma za afya tiba, kinga na kudhibiti taka ngumu na taka maji;
Kutoa huduma ya elimu ya msingi na sekondari;
Kutoa ushauri wa kitaalamu;
Kusimamia utekelezaji wa sheria za nchi na sheria ndogo ndogo za Halmashauri.
Kuratibu shughuli za burudani, michezo na maendeleo ya vijana.
Kuratibu mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
4.0 MISINGI YA UTOAJI HUDUMA
Ili kutekeleza mkataba huu, Halmashauri itazingatia mambo mbalimbali katika kutoa huduma kwa wateja kama yafuatayo:
Kuweka viwango vya huduma
Viwango vya huduma zetu vitawekwa wazi kwa wateja ili waweze kufuatilia na kutathmini utendaji wetu wa kazi.
Kuwa wazi na kutoa taarifa kuhusu huduma
Tutakuwa wazi katika kutoa huduma zetu kwa wateja, kuwasaidia wateja na kuwapatia taarifa zote kuhusu huduma zetu, gharama zetu na mafanikio yetu ya kila mwaka.
Kushirikisha wengine
Tutashirikiana na kushauriana na wateja wetu pamoja na watumishi na kutumia ushauri mzuri utakaotolewa katika kuboresha huduma zetu.
Kuwatendea haki wote
Tutawatendea haki wateja wetu wote, tutaheshimu utu wao, na haki zao binafsi, kuwasaidia kila iwezekanavyo na kutoa kipaumbele kwa wenye mahitaji maalumu.
Kukuza upatikanaji huduma
Tutatoa huduma zetu kwa wateja kwa haraka na kwa urahisi na wateja wetu watapewa fursa ya kuchagua huduma na pia tutakuza matumizi ya teknolojia kadiri ya uwezo wetu.
Kutatua matatizo yanayojitokeza
Tutatatua matatizo yatakayojitokeza haraka iwezekanavyo na malalamiko yote yatakayowasilishwa yatashughulikiwa kwa uwazi.
Matumizi bora ya rasilimali
Tutatumia rasilimali kiufanisi na itakayotoa matunda mazuri kwa walipa kodi, wafadhili na wateja wote.
Kuboresha huduma
Tutatafuta kwa bidii njia bora zaidi za kutoa huduma zetu.
Kushirikiana na watoa huduma wengine
Tutafanya kazi na Wizara, Idara na Wakala mbalimbali pamoja na watoa huduma wengine kuhakikisha kuwa huduma zetu ni rahisi kutumika na bora. Halmashauri ya Manispaa ya Songea inawajibika moja kwa moja kwa masuala ya UKIMWI, usawa na jinsia na mifumo ya utawala ya watumishi wa Umma.
5.0 MAADILI MUHIMU
Ili utumishi wa Halmashauri uwe wenye ufanisi na wa kuheshimika, watumishi wanapaswa kuzifuata kanuni za maadili ya utumishi pamoja na kuwa na tabia na mwenendo unaozingatia mambo yafuatayo:
Kutoa huduma bora.
Utii kwa serikali.
Bidii ya kazi.
Kutoa huduma bila upendeleo.
Staha kwa wananchi.
Uaminifu na
Kuheshimu sheria na Matumizi bora ya taarifa za kazi.
6.0 WATEJA NA MATARAJIO YAO
6.1 WATEJA WETU
Wafuatao ni wateja wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea na matarajio yao ni kama yafuatavyo;
1. Wizara, Idara za Serikali na Wakala wanatarajia:
Mahusiano mazuri.
Ufanisi katika utendaji wa kazi.
2. Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inatarajia:
Utekelezaji na usimamizi wa sera, miongozo, sheria na maelekezo ya serikali kuu.
Mahusiano mazuri; na
Taarifa sahihi.
Kuwa na wataalam wenye sifa na uwezo wa hali juu ili kumudu majukumu makubwa.
3. Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea wanatarajia:
Utawala bora.
Usalama kazini.
Miundo sawa ya kazini inayohamasisha.
Mafunzo.
Mazingira mazuri ya kazi na vitendea kazi vilivyo bora.
Malipo wanayostahili wakati wanapostaafu.
Mfumo mzuri wa kudhibiti nidhamu kazini.
Mwongozo wa wazi na wa kiushindani wa uajiri, uteuzi na upandishaji vyeo.
Mfumo ulio wazi wa utathmini wa utendaji kazi na.
Kanuni na taratibu bora za utawala.
4. Washirika wa maendeleo na wahisani wanatarajia:
Matumizi bora ya pesa zitolewazo
Kutumia misaada kwa kazi zilizopangwa
Kuwepo na uadilifu, utawala bora na umakini wa kazi.
Kupata taarifa ya shughuli za maendeleo wanazochangia kwa wakati, ubora na kwa ukweli.
Kuwa na mipango mizuri ya maendeleo.
Amani, Utulivu na usalama.
Uwajibikaji na uwazi.
5. Jamii inatarajia:
Huduma bora.
Uwazi na utawala bora
Majibu ya kero kwa wakati.
6. Mashirika yasio ya Kiserikali (NGOs) na vikundi vya kijamii (CBOs):
Utawala bora.
Misaada ya kitaalamu na Takwimu sahihi.
Kupata ushauri wa kitaalam.
Kusajiriwa/kupata maombi yao ya kusajiriwa kwa wakati.
Sera na miongozo.
Amani, Utulivu na Usalama.
Ushirikiano na Ushirikishwaji.
7. Vyama vya Siasa vinatarajia:-
Kushirikishwa.
Takwimu sahihi.
Utawala bora.
Uwazi.
Haki sawa kwa wote.
Kuzingatia maoni ya wananchi na Kufanikisha mipango ya serikali.
Kutambua uwepo wa vyama vya siasa
Kushirikishwa katika maamuzi mbalimbali ya Halmashauri
Utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa chama tawala
Amani, Utulivu na Usalama.
Kupewa haki sawa kwenye chaguzi mbalimbali
8. Vyombo vya habari vinatarajia;
Kupata habari zilizokamalika na kwa wakati muafaka
Kupata taarifa za matukio yote kwa uwazi.
Kushirikishwa katika shughuli za maendeleo.
Amani, Utulivu na usalama.
8. Sekta Binafsi zinatarajia:
Huduma bora.
Tafsiri ya Sera na Miongozo.
Kushirikishwa katika kutoa huduma.
9. Taasisi za kidini zinatarajia:
Amani na utulivu.
Mahusiano mazuri.
Kushirikishwa katika kutoa huduma za kijamii.
Kuheshimu uhuru wa kuabudu.
Kutoa haki sawa kwa madhehebu ya kidini
Haki ya kupata vibali ya kufanya mihadhara na mikutano
10. Taasisi za umma zinatarajia:
Huduma bora
Taarifa sahihi
Ushirikiano na mahusiano mazuri
7.0 VIWANGO VYA HUDUMA
7.1 IDARA YA UTUMISHI NA UTAWALA
7.1.1 UTUMISHI NA UTAWALA
NA |
HUDUMA |
MATARAJIO |
1 |
Kutoa miongozo ya utendaji wa kazi na
kuisambaza kwa watumishi. |
Tutatoa miongozo ya utendaji wa kazi ndani ya siku 1 ya kazi.
|
2 |
Kupandisha vyeo vya watumishi.
|
Tutafanya mchakato wa kupandisha vyeo watumishi ndani ya siku 30 za kazi.
|
3 |
Uhamisho wa watumishi kwenda nje ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
|
Tutapitisha maombi ya uhamisho ndani ya siku 3 tangu kuwasilishwa kwa maombi.
|
4 |
Kusikiliza matatizo ya watumishi na shida zao.
|
Tutasikiliza kila siku za kazi.
|
5 |
Kuhakikisha watumishi wote wanajaza Fomu za OPRAS.
|
Siku 20 za kazi.
|
6 |
Kuidhinisha likizo na madai ya malipo ya likizo ya watumishi.
|
Siku 7 za kazi.
|
7 |
Kuandaa mafao ya wastaafu
|
Tutandaa ndani ya siku 1 ya kazi
|
8 |
Kuandaa mpango wa mafunzo kwa watumishi na madiwani.
|
Mpango utaandaliwa ndani ya siku 14 za kazi.
|
9 |
Kushughulikia uteuzi wa watumishi wanaotakiwa kwenda masomoni.
|
Siku 14 za kazi.
|
10 |
Kufuatilia kadi za bima ya afya kwa ajili ya kuwapatia watumishi.
|
Tutafuatilia ndani ya siku 1 ya kazi.
|
11 |
Kushughulikia na kuomba kibali cha ajira mpya.
|
Ajira mpya zitashughulikiwa ndani ya siku 30 za kazi.
|
12 |
Kutafuta na kupeleka jalada kwa afisa anayetakiwa kulishughulikia.
|
Dakika 30 tangu ombi kupokelewa masjala kuu ya Halmashauri.
|
13 |
Kushughulikia barua za maombi mbalimbali yanayoletwa idarani.
|
Maombi yatashughulikiwa ndani ya siku 3 tokea maombi kuwasilishwa.
|
14 |
Kuandaa bajeti ya mishahara ya watumishi wa Halmashauri.
|
Bajeti itaandaliwa ndani ya siku 30 za kazi.
|
15
|
Kutoa tafsiri ya sera, kanuni na taratibu za utumishi kwa watumishi wa Halmashauri.
|
Tafsiri itatolewa ndani ya siku 2 ya kazi.
|
16
|
Kuandika barua za kuwatambulisha watumishi katika taasisi mbalimbali.
|
Barua itaandikwa ndani ya siku 1 mara tu baada ya kuwasilishwa ombi.
|
17
|
Kutunza usafi wa mazingira ya ofisi yetu.
|
Usafi utafanyika kila siku ya kazi.
|
18
|
Kuhifadhi barua zinazoingia Halmashauri katika mafaili.
|
Siku 1 ya kazi mara tu baada ya kupokea barua.
|
19
|
Kusambaza barua kwa wahusika na idara mbalimbali.
|
Siku 2 za kazi toka barua kupokelewa.
|
20
|
Kupeleka hundi katika taasisi.
|
Siku 1 ya kazi mara baada ya hundi kuwa tayari.
|
21
|
Kukagua vyeti vya waajiriwa wapya kama ni halali.
|
Ukaguzi wa vyeti utafanyika ndani ya siku1 ya kazi ambayo mtumishi mpya ameripoti kazini.
|
22
|
Kushughulikia mirathi za watumishi waliofariki kwa kujaza fomu na kuzipeleka kunakohusika.
|
Mirathi itashughulikiwa ndani ya siku 14 za kazi.
|
23
|
Kuandika ripoti ya taarifa za kazi ya mwezi.
|
Siku 1 ya kazi.
|
24
|
Kuandaa taarifa za utendaji wa kazi za robo mwaka
|
Siku 3 za kazi.
|
25
|
Kufuatilia na kupanga matumizi ya magari ya Halmashauri.
|
Siku 1 ya kazi.
|
26
|
Kushughulikia masuala ya nidhamu, baada ya vielelezo vyote muhimu kukamilika.
|
Siku 1 ya kazi mara baada ya tatizo kufikishwa idarani.
|
27
|
Kushughulikia upatikanaji wa vitendea kazi vya ofisi za Halmashauri.
|
Siku 2 za kazi.
|
28
|
Kushughulikia upatikanaji wa chakula na pesa kwa ajili ya watumishi wanaoishi na virusi vya UKIMWI.
|
Siku 7 za kazi.
|
29
|
Kuandaa zawadi za watumishi bora wa Halmashauri.
|
Siku 7 za kazi.
|
30
|
Kuandaa orodha ya madiwani kwa ajili ya malipo ya kila mwezi.
|
Siku 1 ya kazi.
|
31
|
Kusaini mikataba ya Halmashauri na sekta binafsi.
|
Siku 1 ya kazi.
|
32
|
Kuidhinisha malipo ya mishahara ya watumishi wa Halmashauri.
|
Siku 2 za kazi
|
33
|
Kuandaa ratiba ya vikao vya Halmashauri.
|
Siku 1 ya kazi.
|
34
|
Kutawanya ratiba ya vikao kwa madiwani na wakuu wa idara.
|
Siku 1 ya kazi.
|
35
|
Kuandika muhtasari wa vikao vya madiwani na watendaji.
|
Siku 2 za kazi mara baada ya kikao kuisha.
|
36
|
Kutawanya taarifa za vikao kwa wajumbe.
|
Siku 2 za kazi.
|
37
|
Kuandaa na kufuatilia majibu ya utekelezaji wa maazimio yaliyowekwa katika vikao.
|
Siku 14 za kazi.
|
38
|
Kuandaa posho na mahitaji yote ya vikao vya madiwani na watendaji.
|
Siku 1 ya kazi.
|
39
|
Kukamilisha maandalizi ya Bajeti ya Mishahara.
|
Siku 30 za kazi
|
40
|
Kuwasilisha Bajeti ya Mishahara Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
|
Siku 15 kwa kuzingatia mwongozo.
|
41
|
Kutunza kumbukumbu sahihi za watumishi.
|
Kila siku za kazi.
|
7.1.2 KITENGO CHA MALALAMIKO
NA |
HUDUMA |
MATARAJIO |
1 |
Kupokea na kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi na watumishi.
|
Kila siku ya kazi.
|
2 |
Kutatua malalamiko na kero za wananchi na watumishi.
|
Siku 2 za kazi kwa kero ndogo
ndogo na siku 30 kwa kero kubwa. |
3 |
Kutatua kero za kutupa takataka miferejini na maeneo yasiyoruhusiwa.
|
Siku 1 ya kazi.
|
4 |
Kutatua kero kwa kuelimisha wananchi anachotakiwa kufanya.
|
Dakika 10 katika siku ya kazi
|
5 |
Kushughulika malalamiko ya wananchi kuhusu kutokuwepo na huduma za jamii.
|
Kila siku ya kazi
|
6 |
Kuwasilisha taarifa za kero na malalamiko kwa Mkurugenzi Mtendaji na Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
|
Kila robo mwaka
|
7 |
Kupitia taarifa za malalamiko na Kamati za Maendeleo za Kata 21 na Mitaa 79.
|
Kila mwezi na Kila robo mwaka.
|
7.1.3 KITENGO CHA SHERIA
NA |
HUDUMA |
MATARAJIO |
1 |
Kumshauri Mkurugenzi wa Halmashauri kuhusu mambo ya kisheria.
|
Kila siku za kazi.
|
2 |
Kushughulikia kesi mahakamani za kushtaki au kushtakiwa Halmashauri.
|
Kila siku za kazi kesi inapotajwa
Katika mahakama husika |
3 |
Kusaini fomu za dhamana.
|
Dakika 3.
|
4 |
Kutunga rasimu za sheria ndogo ndogo za Manispaa ya Songea.
|
Siku 60 za kazi.
|
5 |
Kutunga sheria ndogo ndogo za kila idara
|
Siku 60 za kazi.
|
6 |
Kutayarisha mikataba ya Halmashauri.
|
Siku 7 kwa kila mkataba.
|
7 |
Kufuatilia utekelezaji wa sheria ndogo ndogo na kuandika taarifa.
|
Siku 2 za kazi.
|
8 |
Kuandaa bajeti ya mabaraza ya kata.
|
Siku 7 za kazi.
|
9 |
Kuwafundisha wajumbe wa mabaraza ya kata juu ya kanuni na taratibu uendeshaji wa mabaraza.
|
Siku 2 za kazi mara baada ya kuteuliwa.
|
10 |
Kumshauri Mkurugenzi na watendaji wake mambo ya kisheria katika vikao vya uongozi.
|
Kila siku ya vikao.
|
7.1.4 KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI
NA |
HUDUMA |
MATARAJIO |
1 |
Kukagua na kutoa taarifa ya mapato ya Halmahauri ili kuhakikisha taratibu za fedha zimefuatwa.
|
Siku 1 ya kazi kila robo mwaka.
|
2 |
Kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya Halmashauri kama taratibu zimefuatwa (Value forMoney).
|
Siku 1 ya kazi kwa kila mradi.
|
3 |
Kukagua mikataba ya wakandarasi kama taratibu za fedha na nyaraka zilizoambatanishwa zinakidhi kanuni na taratibu za fedha za serikali.
|
Siku 2 za kazi.
|
4 |
Kukagua risiti za urejeshaji masurufu.
|
Siku 1 ya kazi.
|
5 |
Kumshauri Mkurugenzi wa Halmashauri kuhusu taratibu za matumizi ya fedha serikali.
|
Kila siku za kazi.
|
6 |
Kufanya uchunguzi maalum kuhusu matumizi mabaya ya fedha (Special Checks and Investigation).
|
Siku 7 za kazi
|
7 |
Kushughulikia masuala ya ukaguzi wa miradi (Performance Appraisal of Development Project).
|
Siku 1 ya kazi kwa kila mradi
|
8 |
Kuandaa ratiba za muda mrefu za shughuli za ukaguzi.
|
Siku 1 ya kazi kwa kila mwaka
|
9 |
Kumshauri Afisa Mhasibu kuhusu mabadiliko ya miongozo ya ukaguzi (Audit Guides) na kupendekeza mfumo mzuri wa udhibiti wa ndani (Internal Control).
|
Siku 2 za kazi kwa kila robo mwaka
|
10 |
Kufanya tathimini juu ya ufanisi (Effectiveness) katika ngazi zote za utawala kwenye Halmashauri ili kuona namna wanavyosimamia mali (Resources) na pia kuona kama taratibu zinafuatwa.
|
Siku 1 ya kazi kwa kazi moja ya Utawala kwa mwezi mmoja
|
11 |
Kufanya uhakiki na kutoa taarifa juu ya udhibiti wa ukusanyaji mapato na utunzaji wa fedha za Halmashauri.
|
Siku 1 ya kazi kwa kila wiki
|
7.1.5 KITENGO CHA MANUNUZI
NA |
HUDUMA |
MATARAJIO |
1 |
Kuomba kibali cha kununua bidhaa kutoka kwa maafisa wanaohusika kwa kujaza fomu.
|
Dakika 5 za kazi.
|
2 |
Kujaza fomu zinazoonyesha bidhaa zinazohitajika na kusainiwa na mkuu wa kitengo.
|
Dakika 5 za kazi.
|
3 |
Kutangaza zabuni katika magazeti.
|
Siku 2 za kazi.
|
4 |
Kuchagua wazabuni watakaotoa huduma katika Manispaa.
|
Siku 60 za kazi.
|
5 |
Kumkabidhi mzabuni nyaraka zinazoonyesha aina za bidhaa zinazohitajika.
|
Siku 1 ya kazi.
|
6 |
Kupokea bidhaa zilizonunuliwa na mzabuni na kuweka stoo.
|
Siku 1 ya kazi.
|
7 |
Kupeleka nyaraka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ili aidhinishe malipo.
|
Dakika 60 za kazi.
|
8 |
Kuwaatarifu wazabuni waonyeshe gharama za kutoa huduma.
|
Siku 1 ya kazi.
|
9 |
Kufungua na kutangaza bei zilizotolewa na wazabuni.
|
Masaa 2 ya kazi.
|
10 |
Kuteua wajumbe watakao tathmini maombi ya dhabuni na kumpata mshindi.
|
Siku 14 za kazi.
|
11 |
Kumpatia barua na mkataba mzabuni aliyeshinda.
|
Siku 14 za kazi baada ya kujulishwa washiriki wenzake
|
12 |
Kuandaa matangazo ya manunuzi.
|
Siku 4 za kazi
|
13 |
Kuandaa mikataba yote ya manunuzi.
|
Siku 30 za kazi
|
14 |
Kutunza rejesta ya mikataba yote ya manunuzi.
|
Siku 365 za kazi
|
15 |
Kusimamia na kuhakikisha taratibu zote za manunuzi zinafuata.
|
Siku 365 za kazi
|
16 |
Kusimamia manunuzi.
|
Siku 365 za kazi
|
7.1.6 KITENGO CHA UCHAGUZI
NA |
HUDUMA |
MATARAJIO |
1 |
Kusimamia na kuratibu zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la kupiga kura kadri ya maelekezo ya Tume ya Taifa ya uchaguzi.
|
Siku 60 za kazi au kadri itakavyoelekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
|
2 |
Kusimamia chaguzi mbalimbali zikiwemo za Serikali Kuu na TAMISEMI.
|
Siku 90 za kazi au kadri itakavyoelekezwa na Tume ya Uchaguzi/TAMISEMI
|
3 |
Kutunza na kuhifadhi vifaa na nyaraka zote za uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya uchaguzi.
|
Siku 365 za kazi
|
4 |
Kuratibu shughuli za uchaguzi mdogo itokeapo nafasi wazi kutokana na sababu mbalimbali.
|
Siku 60 za kazi
|
6 |
Kuandaa na kutoa taarifa kuhusu nafasi wazi na sababu zake.
|
Siku 7 za kazi
|
5 |
Kuandaa na kutoa mafunzo ya uchaguzi kwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura.
|
Siku 7 za kazi au kadri itakavyoelekezwa na Tume ya Uchaguzi/TAMISEMI
|
6 |
Kuwalisisha taarifa ya mwenendo wa uchaguzi uliofanyika/Matokeo Tume ya Taifa ya uchaguzi.
|
Siku 2 za kazi
|
7.1.7 KITENGO CHA TEHAMA
NA |
HUDUMA |
MATARAJIO |
1 |
Kuwepo kumbukumbu za taratibu za kisasa na mbinu za kufanyia kazi.
|
Miezi 5 ya kazi
|
2 |
Kutekeleza chati za mtiririko wa mifumo ya nyendo za taarifa na uthibiti unaohusu Kompyuta.
|
Siku 5 za kazi
|
3 |
Kutoa msaada wa kiufundi Ofisi mbalimbali za Halmashauri.
|
Siku 5 za kazi
|
4 |
Kuandika miongozo kwa watuniaji na mfumo.
|
Siku 6 za kazi
|
5 |
Kufuatilia mfumo wa usalama wa kompyuta.
|
Siku 5 za kazi
|
6 |
Kutoa msaada wa kiufundi kwa watumiaji wa kompyuta.
|
Siku 5 za kazi
|
7.1.8 KITENGO CHA NYUKI (MALIASILI)
NA |
HUDUMA |
MATARAJIO |
1 |
Kuotesha miti mbalimbali.
|
Miezi 5 ya kazi.
|
2 |
Kuhamasisha upandaji miti kwa kufanya mikutano na jamii.
|
Siku 1 ya kazi kwa kata.
|
3 |
Kuelimisha jamii kuhusu sheria za misitu.
|
Siku 7 za kazi.
|
4 |
Kufanya maonyesho ya nanenane.
|
Siku 10 za maonyesho.
|
5 |
Kutoa elimu ya matumizi ya zana sahihi za uvuvi.
|
Siku 14 za kazi kila elimu inapotolewa.
|
6 |
Kuelimisha jamii kuhusu sera na sheria zinazohusu wanyamapori.
|
Siku 14 za kazi
|
7 |
Kuelimisha jamii jinsi ya kudhibiti wanyama wakali na waharibifu wa mazao kwenye kata ambazo wanyama hao wanaonekana.
|
Siku 14 za kazi.
|
8 |
Doria ya maliasili katika misitu na uvuvi.
|
Siku 48 kila mwaka.
|
7.1.9 KATA
NA |
HUDUMA |
MATARAJIO |
1 |
Mtendaji wa kata kusikiliza kero na malalamiko na kuyatatua.
|
Siku 1 ya kazi.
|
2 |
Kusimamia utekelezaji wa miradi ya mendeleo katika kata.
|
Kila siku za kazi.
|
3 |
Kusimammia na kukagua usafi wa mazingira katika kata.
|
Siku 1 ya kazi katika kila kata.
|
4 |
Kuhamasisha ulinzi na usalama kwa kufanya mikutano.
|
Siku 1 ya kazi kila
|
5 |
Kuhakikisha watendaji wa mitaa wanasimamia ulinzi na usalama katika mitaa yao.
|
Siku 1 ya kazi kila baada ya
miezi miwili. |
6 |
Kusimamia chaguzi za serikali za mitaa na serikali kuu.
|
Kipindi chote cha uchaguzi.
|
7 |
Kusimamia uandikishwaji wa wapiga kura.
|
Kipindi chote cha uandikishwaji wa wapiga kura.
|
8 |
Kufuatilia utoaji wa huduma za jamii katika kata.
|
Siku 1 ya kazi kwa kila sekta.
|
7.2 IDARA YA FEDHA NA BIASHARA
7.2.1 SEKSHENI YA FEDHA
NA |
HUDUMA |
MATARAJIO |
1 |
Kulipa wazabuni.
|
Siku 30 za kazi tangu kupokea maombi ya malipo
|
2 |
Kulipa mishahara baada ya kupokea kutoka Hazina.
|
Siku 5 za kazi baada ya TT ya mishahara kuingizwa benki.
|
3 |
Kutayarisha na kulipa posho mbalimbali kwa watumishi na madiwani.
|
Siku 5 za kazi.
|
4 |
Kulipa fedha ya likizo ya watumishi wa Halmashauri.
|
Ndani ya siku 5 malipo yatalipwa.
|
5 |
Kupokea mapato ya Halmashauri.
|
Kila siku ya kazi.
|
6 |
Kufuatilia kodi mbalimbali kwenye maeneo husika kwa wateja ambao hawajalipa.
|
Kila siku ya kazi.
|
7 |
Kutoa elimu kwa walipa kodi kuhusu kodi mbalimbali wanazotakiwa kulipa.
|
Kila siku ya kazi.
|
8 |
Kusimamia na kuthibiti masuala yote ya mapato na matumizi ya Halmashauri.
|
Kila siku ya kazi.
|
9 |
Kuandaa malipo mbalimbali ya wateja wa ndani na wateja wa nje.
|
Siku 3 za kazi
|
10 |
Kurejesha asilimia 10 ya ukusanyaji mapato yenye vielelezo kwa wakusanyaji wa ndani.
|
Siku 5 za kazi
|
11 |
Kujibu hoja za Mkaguzi wa ndani na wakaguzi wa nje.
|
Siku 14 za kazi kuanzia tarehe ya kukabidhiwa hoja.
|
7.2.2 SEKSHENI YA BIASHARA
NA |
HUDUMA |
MATARAJIO |
1 |
Kutoa leseni za biashara na vileo.
|
Siku 1 ya kazi.
|
2 |
Kukagua leseni za biashara na vileo.
|
Dakika 5 kwa kila Biashara.
|
3 |
Kukagua leseni za nyumba za kulala wageni.
|
Dakika 5 kila nyumba ya kulala wageni.
|
4 |
Kukagua nyumba za kulala wageni kuhusu ushuru wa malazi.
|
Dakika 60 kwa kila nyumba ya kulala wageni.
|
5 |
Kutoa ushauri wa wafanyabiashara kuhusu uendeshaji biashara.
|
Dakika 60 kwa kila biashara.
|
6 |
Kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu sera, sheria, na kanuni za kufanya biashara
|
Siku 4 za kazi kwa kila kikundi chawafanyabiashara.
|
7.3 IDARA YA MIPANGO, TAKWIMU NA UFUATILIAJI
NA |
HUDUMA |
MATARAJIO |
1 |
Kuandaa Bajeti ya Halmashuari ya Manispaa ya Songea.
|
Siku 90 za kazi.
|
2 |
Kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Manispaa ya Songea.
|
Siku 7 za kazi.
|
3 |
Kukusanya takwimu kuhusu hali ya kiuchumi ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
|
Siku 90 za kazi.
|
4 |
Kukusanya takwimu za mfumo wa ufuatiliaji na tathmini za serikali za mitaa.
|
Siku 30 za kazi.
|
5 |
Kutoa ushauri kwa jamii kuhusu tafiti na takwimu.
|
Siku 7 za kazi.
|
6 |
Kuchambua sera za kitaifa na kuzifikisha ngazi za chini.
|
Siku 7 za kazi.
|
7 |
Kuratibu mafunzo ya uimarishaji mipango na ushirikishwaji jamii katika kupanga mipango ya maendeleo na utekelezaji wake.
|
Siku 30 za kazi.
|
8 |
Kuandaa taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kila robo mwaka.
|
Siku 7 za kazi.
|
9 |
Kuratibu upimaji wa Halmashauri dhidi ya masharti ya kupata fedha za maendeleo.
|
Siku 30 za kazi.
|
7.4 IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
NA |
HUDUMA |
MATARAJIO |
1 |
Kuelimisha jamii na wanawake kuhusu sera ya jinsia.
|
Siku 2 za kazi.
|
2 |
Kutoa mikopo kwa akina mama na vijana.
|
Ndani ya siku 14.
|
3 |
Kuhakikisha mipango ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea inazingatia jinsia.
|
Siku 1 za kazi.
|
4 |
Kuandaa mpango wa idara.
|
Siku 14 za kazi.
|
5 |
Kupokea mipango kutoka kila kata ya Manispaa ya Songea.
|
Siku 1 ya kazi kwa kila kata.
|
6 |
Kuandaa taarifa ya mwezi ya Idara
|
Siku 2 za kazi.
|
7 |
Kuandaa takwimu za shughuli za maendeleo.
|
Siku 1 ya kazi.
|
8 |
Kuratibu shughuli za asasi zisizo za kiserikali
|
Siku 1 ya kazi.
|
9 |
Kutoa misaada ya fedha na chakula kwa waathirika wa Virusi vya UKIMWI.
|
Siku 7 za kazi.
|
10 |
Kutoa ushauri nasaha kwa muathirika wa Virusi vya UKIMWI.
|
Siku 1 ya kazi.
|
11 |
Kutoa mafunzo ya kuhusu UKIMWI kwa jamii na watumishi Manispaa ya Songea.
|
Siku 3 za kazi.
|
12 |
Kutoa mafunzo kwa vijana juu ya stadi za maisha
|
Siku 14 za kazi.
|
13 |
Kusimamia miradi ya vijana.
|
Siku 1 ya kazi.
|
14 |
Kusimamia vijana ili wapate mikopo na kurejesha.
|
Siku 7 za kazi.
|
15 |
Kusimamia uanzishwaji wa SACCOS za vijana kwa kuwaunganisha na kuwaeleza umuhimu wa SACCOS.
|
Siku 7 za kazi.
|
16 |
Kutambua maeneo ambayo yanaweza kutokea maafa.
|
Siku 14 za kazi.
|
18 |
Kupitia TASAF kusaidia mitaji katika makundi maalumu.
|
Siku 180 za kazi.
|
20 |
Kuratibu shughuli za baraza la watoto.
|
Siku 2 za kazi.
|
21 |
Kuratibu shughuli za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
|
Siku 1 ya kazi.
|
22 |
Kuelimisha jamii na watoto kuhusu sera ya watoto.
|
Siku 2 za kazi.
|
23 |
Kutayarisha taarifa za watoto kutoka katika kila kata.
|
Siku 30 za kazi.
|
24 |
Kuelimisha jamii kuhusu haki za watoto na wajibu wa mtoto.
|
Siku 4 za kazi.
|
SEHEMU YA KITUO CHA KULELEA WATOTO
NA |
HUDUMA |
MATARAJIO |
1 |
Kukagua jengo na eneo la kituo kipya cha kulelea watoto.
|
Siku 14 za kazi.
|
2 |
Kuwasilisha taarifa za kituo cha kulelea watoto kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea.
|
Siku 1 ya kazi.
|
3 |
Kuwasilisha maombi ya kufungua kituo cha kulelea watoto kwa Mkurugenzi.
|
Siku 30 za kazi baada ya kpokea maombi.
|
4 |
Kutoa taarifa kwa mteja kuhusu kukataliwa au kukubaliwa kuanzishwa kituo cha kulelea watoto.
|
Siku 7 za kazi.
|
5 |
Kukagua kituo cha kulelea`watoto kinavyotoa huduma.
|
Siku 1 ya kazi kila baada ya miezi 3.
|
SEHEMU YA HAKI ZA WATOTO
NA |
HUDUMA |
MATARAJIO |
Matangazo
Habari Mpya
VideoTovuti Mashuhuri
Idadi ya Wasomaji DunianiIdadi ya WasomajiRamani ya MahaliWasiliana nasiSONGEA MUNICIPAL COUNCIL Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA Simu ya Mezani: 025 2602970 Simu ya Kiganjani: Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa |