MRADI wa maji katika Mtaa wa Ruhuwiko Kanisani Kata ya Ruhuwiko Manispaa ya Songea mkoa wa Ruvuma, uliibuliwa na Wananchi wenyewe mwaka wa fedha 2013/2014 na kuanza kujengwa mwaka wa fedha 2014/2015,Mkandarasi akiwa ni Girafe Investment Company.
Mhandisi wa Maji katika Manispaa ya Songea Samwel Sanya anasema ujenzi wa mradi huu ulikadiria kugharimu kiasi cha zaidi ya sh.milioni 488.
Kwa mujibu wa Mhandisi Sanya hadi sasa Mkandarasi amelipwa zaidi ya milioni 421 na kwamba kiasi cha fedha ambacho kimebakia ni zaidi ya milioni 67.
Hata hivyo amesema mkataba umekwisha ambapo mradi huo umeanza kutoa huduma kwa wananchi na kwamba bado mradi huo upo kwenye hatua za matazamio
Hata hivyo anasema hadi kukamilika kwa Mradi huo mwaka wa fedha 2016/2017 mradi uligharimu kiasi cha sh.milioni 394.7ambazo zilitumika katika Ujenzi wa miundombinu ya maji.
Sanya anazitaja changamoto za mradi huo kuwa ni Manispaa kutopata fedha za kukamilisha mradi toka serikali kuu kwa wakati hali iliyochelewesha mradi kukamilika kwa wakati na wananchi kuwa na uelewa mdogo wa uchangiaji na uendeshaji wa miradi ya maji.
Ili kuhakikisha kuwa mradi unakuwa endelevu Sanya anasema Manispaa ya Songea itakabidhi mradi huu kwa Mamlaka ya Maji safi na maji taka Manispaa ya Songea(SOUWASA) ambao watasaidia katika uendeshaji wa mradi wa maji kwa kushirikiana na Mtaa wa Ruhuwiko Kanisani walioibua mradi huo.
Watu wapatao 3,447 kutoka katika Mtaa wa Ruhuwiko Kanisani wanatarajia kunufaika na mradi huo wa maji safi na salama baada ya mradi kukamilika,
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa