Shirika la Afya Duniani (WHO) limethibitika kuwepo mlipuko wa ugonjwa wa ebola katika nchi ya Kongo DRC kupitia vipimo vya maabara baada ya kutokea wagonjwa27 na 17 kati yao wamefariki dunia.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amekiri kupata taarifa kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),hata hivyo amewataka watanzania kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo hatari ili usiingie katika nchi yetu.
“Ugonjwa wa Ebola ni hatari na unasambaa kwa kasi na kuleta madhara makubwa kwa afya duniani (Public Health Emergence of International Concern), lakini hadi sasa hapa nchini hakuna mgonjwa aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa na virusi vya ebola,“alisema Ummy.
Amesema Wizara inatoa tahadhari ya ugonjwa huo kwa mikoa yote hasa inayopakana na nchi jirani ya Kongo DRC ikiwemo Kigoma,Rukwa,Songwe,Kagera,Mwanza,Katavi
BOFYA HAPA KUFAHAMU .JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA EBOLA.pdf
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa