UGONJWA WA AJABU WAWAKUMBA WANAFUNZI 335
UGONJWA wa ajabu umezuka katika shule ya msingi Subira iliyopo katika manispaa ya Songea mkoani Ruvuma tangu Machi mwaka huu umesababisha wanafunzi 335 kutohudhuria shule hivyo kukosa masomo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Majidu Ngonyani amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 578 lakini wanafunzi wanaohudhuria masomo ni 243 ambao ni sawa na asilimia 42.
Kwa mujibu wa Ngonyani wanafunzi wanaopata ugonjwa huo ni wa kike na kwamba hadi sasa licha ya madaktari kuchukua vipimo kwa wanafunzi wanaugua bado haijafahamika ni ugonjwa gani.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Alhaji Abdul Hassan Mshaweji na Afisa Elimu Msingi wa Manispaa hiyo Edith Kagomba mara kadhaa wamefanya ziara katika shule hiyo ili kujaribu kutafutia ufumbuzi wa kudumu.
Katika kikao cha Julai 21 mwaka huu,kamati ya shule,walimu na wananchi walikubaliana Ijumaa ya Julai 27 kufanya maombi maalum yaliyoshirikisha madhehebu mbalimbali ya dini ambayo wanaamini yanaweza kumaliza tatizo hilo linaloathiri taaluma katika shule hiyo.
Tatizo lililoikumba shule hiyo limewahi kutokea katika shule ya sekondari Beroya,shule ya msingi Mwengemshindo na Chandarua katika manispaa ya Songea ambayo ufumbuzi wake ulifanywa kwa maombi maalum ya madhehebu ya dini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa