UMAARUFU wa mkoa wa Mtwara katika kula nyama ya panya ni fursa mojawapo ya kuvutia utalii mkoani hapa. Hilo litawezekana iwapo jamii ya watu wanaotumia chakula hicho watawekewa mazingira mazuri ya kujitangaza na kukitangaza chakula hicho kupitia matukio mbalimbali ikiwemo ‘Panya festival’ au panya Choma.
Akizungumza katika kipindi cha safiri nasi kilichokuwa kikirushwa moja kwa moja kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara leo, Mhe. Gelasius Byakanwa amesema hilo ni mojawapo ya malengo yake kuhakikisha fursa mbalimbali za mkoa wa Mtwara ikiwemo ulaji wa nyama ya panya unatumika kama kivutio. Aidha katika ratiba yake amepanga kabla ya mwezi wa saba mwaka huu kuandaa tukio ambalo na yeye atashiriki kula nyama hiyo.
Anasema fursa hiyo inaweza kuwavuta watu wengi kutoka ndani na nje ya nchi na kuufanya mkoa wa Mtwara kujulikana zaidi. Aidha itatoa fursa ya kufanya maboresho katika chakula hicho katika mtindo bora na wa kisasa zaidi.
“Kwa nini tusitangaze, isiwe rasmi kwamba panya ni chakula, tukawakaribisha mikoa mingine kwamba njooni Mtwara tule panya. Lakini kama sisi wenyewe tukikitambua na kukihalalisha kuwa hiki ni chakula bila kuitenga ile jamii… so long as hakina madhara kwa afya ya mtu, na pengine imani yako haizuii, mimi sioni sababu kwa nini tusikichukuwe na chenyewe kikawa kivutio”. Amesema Mhe.Byakanwa.
Mhe. Byakanwa ambaye ni Mwenyeji wa Mkoa wa Kagera ametolea mfano mkoa huo kwamba ni maarufu kwa ulaji wa Senene na kwamba chakula hicho sasa kimevuka mipaka kutoka Bukoba hadi nje ya nchi.
“Kule Bukoba tunakula senene, mwanzoni senene walionekana wanaliwa Bukoba tu lakini sasa kila sehemu wanakula, mpaka wengine wanakuwa exported nje ya nchi. Kwa nini panya nao wasiwe hivyo?
CHANZO CHA HABARI NI TOVUTI YA OFISI YA MKOA WA MTWARA
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa