Mpaka kufikia Desemba 2018 Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imefikia asilimia 50.1 sawa na idadi ya watu 45,929, idadi halisi ya wakazi waishio pembezoni mwa mji 90,728 ambao bado hawajafikiwa na mtandao wa mamlaka ya maji safi na taka (SOUWASA).
Katika mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri inaendelea kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya maji kama ifuatavyo:Visima 49 vimejengwa kati ya visima 60 Kwa gharama ya MkatabaTshs. 1,537,533,400 na Mtandao wa maji ya bomba mita 31.122 umejengwa na vituo vya maji 5 kwa gharama ya mkataba wa Tshs. 681,570,020
Halmashauri ya Manispaa ya Songea inaendelea kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya maji kupitia programu ya maji na usafi wa mazingira awamu ya pili katika Mitaa ya Mwengemshindo, Pambazuko, Mletele, Mjimwema, Makemba, Mdundiko, Nonganonga, Lilambo A, Lilambo B, Liwumbu, Nangwai, Subira Kati, Kisiwani C, Lami na Kihekwa. Katika Mitaa hiyo yote ujenzi wa miundombinu unaendelea na upo hatua mbalimbali ya ujenzi. Miradi hiyo ikikamilika itagharimu kiasi cha Tshs. 3,479, 834,306 na itaongeza upatikanaji wa huduma ya maji kutoka 50.1% hadi kufikia 70.2% na kufanya ongezeko la watu kupata huduma ya maji kutoka 45,929 hadi kufikia watu 64,356.
Lengo la Halmashauri ni kutekeleza Sera ya maji na malengo ya Serikali kutoa huduma ya maji safi na salama kufikia asilimia 85 na zaidi, katika maeneo ya pembezoni mwa Mji ifikapo mwaka 2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa