Mwenyekiti wa kamati ya Lishe Manispaa ya Songea Wakili. Bashiri Muhoja amewataka wataalamu wa idara ya kilimo na mifugo,Mipango, Fedha, Elimu Msingi na Sekondari pamoja na wataalamu idara ya Afya wahakikishe wanasimamia na kutekeleza muongozo wa Mkataba wa Lishe ili kuondoa udumavu na Utapiamlo.
Kauli hiyo imetolewa kwenye kikao cha kamati ya Lishe Manispaa ya Songea kilichofanyika tarehe 15 Mei 2024 kilichohudhuriwa na wakuu wa idara mbalimbali kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa afua za lishe katika kipindi cha Januari hadi Machi 2024.
Amewataka wakuu wa shule, pamoja na bodi za shule kuhakikisha kila mzabuni anayepeleka chakula shuleni ahakikishe anaweka viini lishe, pia kila shule iunde kamati za lishe za shule pamoja na uanzishaji wa bustani za mboga mboga. “ alisema Wakili. Muhoja.”
Kwa upande wake Mganga Mkuu Manispaa ya Songea Dkt. Amos Mwenda amewataka wananchi kuwa na mpango wa uzazi salama kwa mzazi kabla kupanga kushika mimba miezi mitatau kabla ni lazima wapime afya zao ili kukinga magonjwa kwa mtoto atakayezaliwa.
Dkt. Mwenda amesema kuwa utafiti umefanyika kwa wanawake wengi wanaojifungua wengi wao hujifungua watoto wenye uzito pungufu ambao unatokana na baadhi ya wanawake hao kuwa na umri mdogo chini ya miaka 21 ambao umekuwa chanzo kikubwa cha tatizo hilo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa