MAAJABU ya jiwe la Mbuji lililopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma,ni kivutio adimu ambacho kinawashangaza wengi.Kwanza unapoliangalia jiwe hilo kwa mbali linaonekana fupi sana,lakini kadiri unavyolikaribia urefu unaongezeka zaidi,pili ni vigumu kulipanda bila kuwaona wazee wa mila,tatu ni vigumu kulizunguka jiwe hilo bila kufuata taratibu na mila za kabila la wamatengo,
Inaamimika katika jiwe hilo kuna viumbe mfano wa binadamu wafupi vinavyoitwa IBUUTA ambavyo vinaonekana,Iwapo mtalii atapanda jiwe hilo bila kuwatumia wazee wa mila ataadhibiwa hata kupoteza maisha na kamwe hawezi kupanda wala kuzunguka.Jiwe pia hutumika kuwaombea watu wanaosumbuliwa na mapepo.Zamani wazee walikuwa wanapanda juu ya jiwe hilo na kucheza ngoma za asili za kabila la wamatengo.
14034959_850086705125606_5466621799886783357_n.jpg13938376_850084431792500_1069391921850635333_n.jpg14022162_850086581792285_2773465762605420672_n.jpg
Mwandishi ni Albano Midelo
mawasiliano albano.midelo@gmail.com,simu 0784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa