Ni katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa zoezi la ugawaji wa dawa za minyoo ya tumbo na minyoo ya kichocho kwa wanafunzi wenye umri wa miaka 5-14 kwa Shule za Msingi Manispaa ya Songea, ambalo limeanza leo 18.09.2020 na linatarajia kukamilika tarehe 21.09.2020 ambapo linatekelezwa chini ya usimamizi wa walimu kwa kila shule husika.
Afisa wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Frank Komakoma akiwa katika ziara ya kuzitembelea shule zilizopo Manispaa ya Songea kwa ajili ya kuangalia mwenendo mzima wa zoezi la ugawaji dawa za minyoo ya kichocho na minyoo ya tumbo kwa wanafunzi wa Shule za Msingi 91 alisema kuwa ameridhika na maandalizi ya watoto shuleni kwani kila shule imewandaa watoto vizuri kwa kuwa elimisha umuhimu wa kumeza dawa za minyoo ya tumbo na kichocho.
Komakoma aliongeza kuwa utekelezaji wa zoezi hilo unaendelea vizuri kwani kila shule imeandaa mazingira safi ya kugawia dawa na pia walimu wamehakikisha kila mtoto ana pata chakula cha kutosha kabla ya kunywa dawa hizo.
Aliwasisitiza Walimu hao kuendelea kuwa karibu na wanafunzi hao pamoja na kuwapatia elimu ya kuwaondoa hofu baada ya kunywa dawa hizo.
Kumbuka dawa hizo zimetolewa bure kwa wanafunzi bila malipo.
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
18.09.2020
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa