Mhe. Jacquiline Ngonyani Msongozi ameitaka jamii kuakikisha inaimarisha Haki, Usawa na ushirikiano ili kuwatendea haki watoto wenye mahitaji maalumu katika Manispaa ya Songea.
Hayo yamejiri kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani iliyofanyika tarehe 02 Machi 2025 katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu (Usonji) kilichopo Subira.
Aidha katika kuwafariji watoto hao, alitoa zawadi ya sabuni, mafuta ya kupikia, na sukari pia katika kutatua changamoto zinazowakabili watoto hao ameahidi kuleta mashine ya kufulia nguo, pamoja na magodoro.
Kwa upande wa Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Songea Diana Mchonga alianza kwa kutoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea kwa kuwezesha kufanyika kwa zoezi hilo, wadau mbalimbali, ambao walitoa michango yao ili kukamilisha ununuzi wa mahitaji kwa watoto hao ikiwemo na mchle, maharage, mafuta ya kupaka, juice, sabuni na Sukari.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni Wanawake na Vijana tuimarishe Haki na Usawa.
Kilele cha maadhimisho hayo kimkoa yatafanyika tarehe 08 machi 2025 katika uwanja wa Majimaji ambapo itafuatiwa na tafrija ya usiku wa mwanamke ambao utafanyika tarehe 09 machi 2025.
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa