Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano amewataka wananchi wa Manispaa ya Songea kuachana na kilimo cha mazoea na kuanza kulima kilimo chenye tija ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi.
Hayo yametolewa wakati wa uzinduzi wa shamba la zao la viazi mviringo ambalo limefanyiwa utafiti kikundi cha SAGCOT na kubaini zao la viazi mviringo, parachichi linfaa kulimwa katika ardhi ya Songea.
Aliongeza kuwa endapo utazingatia taratibu za kilimo bora cha zao la viazi ambalo kwa Ekari moja ya shamba la zao la Viazi Mviringo hutavunwa TAN 20 kwa kila ekari ambalo ni tija kwa mkulima. “Alibainisha”
Wakizungumza wakulima hao kutoka Madaba, Songea vijijini na manispaa ya Songea ambao wameungana na kuunda kikundi kimoja kinachojishughulisha na kilimo ambapo wamesema “wanaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mradi huo ambao kwasasa unatoa huduma kikanda ambao umewasaidia kupata elimu ya kilimo cha Maparachichi, Viazi mviringo na vitunguu.”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa