VIJANA wanaoshi katika mazingira hatarishi wapatao 51 wamehitimu mafunzo ya kozi fupi katika chuo cha ufundi stadi VETA kilichopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Vijana hao wamefadhiliwa mafunzo hayo kupitia Shrika la PADI kwa ufadhili wa shirika la PACT TANZANIA ambao pia wamewapatia vijana hao vifaa mbalimbali vya kazi kulingana na kozi ambazo wamesomea.
Akisoma risala ya Shirika la PADI kwa niaba ya Mtendaji Mkuu Shirika kilo,Mwakilishi huyo Gift Kilasi amesema ufadhili wa watoto hao ni moja ya miradi ambayo inatekelezwa na USAID kizazi kipya mradi ambao unatekelezwa katika Halmashauri tatu za Wilaya ya Songea ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Songea,Manispaa ya Songea na Halmashauri ya Madaba.
Kilasi amesema PADI inatekeleza mradi huo tangu Juni 2017 ambapo mradi umelenga kuwafikia walengwa wapatao 35,037 ambao ni watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi pamoja na walezi wao ambapo hadi sasa wamefanikiwa kuwafikia walengwa wapatao 31,313 sawa na asilimia 91.
Hata hivyo amesema mradi huo unaendeshwa na wahudumu wa kujitolea wapatao 1017 kwa ajili ya mashauri ya watoto na wahudumu 67 wa kuhudumia vikundi vya kiuchumi na amezitaja huduma ambazo zinatolewa kuwa ni elimu ya malezi na matunzo,elimu ya lishe na tahmini ya hali ya lishe,msaada wa kisaikolojia,ulinzi na usaama wa mtoto,huduma ya afya,elimu na mafunzo ya ufundi stadi,kuboresha hali ya uchumi wa kaya na kuwaunganisha watoa huduma kwa njia ya rufaa.
"Katika kipindi cha mwaka 2018/2019 PADI kwa ufadhili wa PACT TANZANIA limefanikiwa kutoa ufadhili wa mafunzo mbalimbali kwa watoto wanaoshi katika mazingira hatarishi katika chuo cha VETA ambayo ni kozi za ushonaji.uungaji vyuma,ufundi magari,saluni za kike,mapishi,ufundi bomba,useremala na fani nyingine'',anasisitiza Kilasi.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyofanyika Septemba 8 katika viwanja vya VETA alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Songea pololet Mgema ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Pendo Ndumbaro ambaye amelipongeza Shirika la PADI kwa kushirikiana na PACT TANZANIA kufadhili mafunzo hayo ya miezi mitatu kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Kupitia Mashirika hayo Vijana hao wametunukiwa vyeti na kupewa vifaa kulingana na kozi walizosomea ambavyo vitawasaidia kujiajiri na kutoa ajira kwa wengine ambao hawakubahatika kupata fursa hiyo watakaporudi katika maeneo yao.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa