Manispaa ya Songea imejaa Simanzi na Masikitiko makubwa baada ya kutokea kifo cha Mhe. Ajira Rajbu Kalinga aliyekuwa Diwani wa kata ya Mfaranyaki ambaye amefariki Dunia tarehe 06 Mei 2023 katika Hosptali ya BOCHI Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa tarehe 08 Mei 2023 katika Makaburi ya Mfaranyaki Manispaa ya Songea.
Marehemu Mhe. Ajira Kalinga aliwahi kutumikia nafasi ya Udiwani wa Viti Maalmu katika kipindi cha mwaka 2018-2020 pia kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 Marehemu alifanikiwa kugombea nafasi ya Udiwani ambao alishinda katika kata ya Mfaranyaki.
Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano alisema “ Enzi za Uhai wake Mhe. Ajira Kalinga alikuwa Mpiganaji na mpambanaji katika kuwahudumia wananchi wake katika kuleta maendeleo katika kata yake hivyo hamna budi kuyatekeleza mema yote ambayo Marehemu Ajira alianza kuyatekeleza.” alisisitiza.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Kapenjama Ndile alisema “ Marehemu Ajira Kalinga alimfahamu kwa utendaji wake wa kazi uliotukuka ambapo mara ya kwanza alimfahamu akiwa ana siku mbili tangu aanze kazi na mara baada ya kumtembelea ofisini kwake ambapo aliweza kumshirikisha changamoto mbalimbali zinazohusu miundombinu ya shule za msingi na Sekondari katika kata ya Mfaranyaki.”
Ndile amewataka wananchi na Viongozi wote kuendelea kuyaenzi mema na mazuri yote ambayo Marehemu Ajira Kalinga alikuwa ameanza kuyatekeleza pamoja na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kumpa pumziko la milele. Amina.
Kwa upande wake Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro (MB) Waziri wa Katiba na Sheria alitoa salamu za pole kwa familia, wananchi wa Manispaa na CCM, kutoka kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutokea kifo cha aliyekuwa Diwani wa kata ya Mfaranyaki Mhe. Ajira Kalinga.
Dkt. Ndumbaro alisema Kwa masikitiko na huzuni kubwa Chama kimepoteza Kiongozi mahiri, Mpiganaji, Mtetezi wa wananchi, hivyo hatuna budi kumuombea apumzike amani.” Alihuzunika”
Alisisitiza wakati tunaombeleza tutafakari mema mazuri ambayo marehemu aliyaanza kuyatekeleza na baadhi yake yataanza kutelezwa hivi karibuni ikiwemo na barabara kiwango cha Lami.
Naye kwa upande wake Komredi Oddo Mwisho Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi amewataka Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa kata kuhakikisha wanasimamia na kuendeleza shughuli zote zilizokuwa zikitekelezwa na Marehemu Mhe. Ajira Kalinga.
Innalillahi wanailillahi Raijun.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa