Halmashauri ya Manispaa ya Songea kupitia Baraza lake Tukufu la Madiwani kwa mwaka wa fedha 2022/2023 liliidhinisha Bajeti pamoja na kuadhimia kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha kununa VISHIKWAMBI kwa ajili ya matumizi ya Madiwani na Wakuu wa Idara na Vitengo katika uendeshaji wa shughuli za vikao vya Menejimenti, Vikao vya Halmashauri pamoja na vikao vya Baraza la Madiwani ili kupunguza matumizi ya karatasi.
HATUA hiyo imetekelezwa kwa asilimia 100% ambapo Halmshauri imeweza kununa na kugawa Vishikwambi 50 vyenye thamani ya zaidi ya Mil. 20 kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji wa Rasilimali za Umma.
Zoezi hilo limefanyika jana tarehe 17 Mei 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea lililoendana na utaoaji wa Mafunzo elekezi ya matumizi sahihi ya mfumo wa TEHAMA na utunzaji wa nyaraka za Serikali yalihudhuriwa na Madiwani, Viongozi ngazi ya Wilaya na Wakuu wa Idara.
Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano alisema “ Vishikwambi vitasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa Taasis, uhakika wa upatikanaji wa taarifa, pamoja na urahisishaji wa utendaji wa kazikwa haraka. Alipongeza.
Mhe. Mbano amewataka Waheshimiwa Madiwani kuzingatia kanuni na taratibu za utunzaji wa siri wa nyaraka za Serikali pamoja na kifaa chenyewe ili mara baada ya kukoma madaraka ya uongozi kila aliyepewa kishikwambi atatakiwa kukikabidhi mikononi mwa Serikali. “ Mbano amesisitiza. “
Kwa upande Mkurugenzi Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko alisema “ Katika kutekeleza agizo hilo Manispaa ya Songea imenunua Vishikwambi 50 na kuvikabidhi kwa Waheshimiwa Madiwani na Wakuu wa Idara na Vitengo kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na kuachana na matumizi ya karatasi na kwenda Digital ( Serikali Mtandao). DKT. Sagamiko “Alishukuru”.
Kwa upande wake Afisa TEHAMA Manispaa ya Songea Mvano Mbalae alisema Mafanikio ya Tehama yatasaidia Kuongeza mapato ya serikali, kupunguza gharama vikao kupitia mikutano ya kimtandao, nakupunguza gharama za uendeshaji wa vikao kwa kutumia vifaa vya tehama vinavyotumia nyaraka laini badala ya nyaraka ngum Ili kulinda na miundombinu ya nyaraka za Tehama Serikali imeandaa Sera na Miongozo ya Usimamizi ambayo ipo kisheria ukiukwaji wa Miongozo hiyo ni Uvunjivu wa Sheria.
Mvano alisema Miongoni wa Sera hizo ni pamoja na Sera ya Tehama (ICT policy), Sera ya kwa Mtumiaji wa Tehama(ICT use Acceptable Policy) Sera ya Ulinzi (ICT security Policy) na Mwongozo wa Matumizi Bora Sahihi na Salama Mifumo na Miundombinu ya Tehama. Alibainisha.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti waheshimiwa Madiwani hao ambapo walianza kwa kuipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha kanuni na sheria na miongozo ya Matumizi sahihi ya TEHAMA ambayo inazitaka Taasis kutumia Vishikwambi na kuachana na Matumizi ya karatasi kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji wa rasilimali za umma na upotevu wa nyaraka. “ Walishukuru. “
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa