SHIRIKA la Afya Duniani(WHO) linabainisha kuwa kuna watu bilioni 1.3 ambao ni moja ya tano ya watu wote duniani wanakosa maji safi na salama ya kunywa.Mwenyekiti wa Baraza la Maji Duniani Loic Fauchon anakiri hivi sasa hali ya upatikanaji wa maji duniani ni mbaya na kwamba watu wengi wanaweza kuangamia kwa kukosa maji safi na salama kutokana na uchafuzi wa vyanzo vya maji unaoendelea duniani kote.
"Leo tunajadili suala la maji ambalo linawatia watu wasiwasi, na linaweza kusababisha migogoro na vita vya kugombania maji vya Dunia.Hivi sasa rasilimali ya maji ipo hatarini kutoweka,binadamu wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji'',anasema Fauchon.Kwa mujibu wa WHO,Watu waliokufa mwaka 2014 kutokana na uchafuzi wa maji, ni mara 10 ya waliokufa kutokana na vita.
Nchi ya Somalia inakabiliwa na ukame wa kutisha ambapo watu milioni sita kati ya milioni kumi wapo katika vita ya kugombania maji na chakula baada ya vyanzo vingi vya maji kukauka na kusababisha njaa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.Matumizi ya maji duniani yameongezeka mara sita zaidi kati ya mwaka1900 na 1995 zaidi ya mara mbili ya kiwango cha ongezeko la watu na huendelea kukua kadri kilimo viwanda na matumizi ya nyumbani yanavyoongezeka. Kilimo hutumia takribani asilimia 70 ya matumizi yote ya
maji duniani.
Ripoti ya Water Aid ina inazitaja nchi ambazo zina hali mbaya zaidi katika huduma ya maji kuwa ni Papua New Guine, Msumbiji , Madagascar na Angola ambayo inangoza ikiwa na asilimia 71 ya wananchi wake wa vijijini wakikosa maji safi na salama.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa