Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mkoa wa Ruvuma imeendesha zoezi la uzinduzi wa kugawa vitambulisho vya Taifa 453,867 ambavyo vimezalishwa hivi karibuni kwa wananchi na wakazi wa Wilaya tano 5 Mkoa wa Ruvuma ambazo ni Songea, Mbinga, Nyasa, Namtumbo na Tunduru.
Zoezi hilo limezinduliwa leo tarehe 15 Disemba 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban Thomas ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile, lililofanyika katika Ukumbi wa ofisi ya kata ya Bombambili Wilaya ya Songea.
Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amewataka kutoa taarifa sahihi wakati wanapojiandikisha kitambulisho cha uraia nakutotoa taarifa sahihi ni kosa kwa mujibu wa sheria.
Amesema kitambulisho cha Taifa ni nyaraka muhimu ya nchi ambacho hutoa taarifa sahihi zenye kuonesha jina, sehemu aliyozaliwa, na uraia wa nchi gani pia amewataka kutunza vitambulisho hivyo kwa kutoa nakala ya kitambulisho na kukitunza ili kuzuwia upotevu wa kitambulisho husika.
Akibainisha takwimu za vitambulisho vilivyozalishwa Mkoani Ruvuma 453,867 ikiwa wilaya ya Songea vitambulisho 139,321, Nysa 37,617, Mbinga vitambulisho 107,577, Tunduru vitambulisho 108,891, Namtumbo vitambulisho 60,461.
IMEANDALIWA NA,
AMINA PILLY,
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa