Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amewataka Maafisa Ugani wa kilimo Wilaya ya Songea wahakikishe wanatekeleza wajibu wao katika kusimamia wakulima na kutoa elimu kwa wananchi juu ya kilimo bora.
Hayo yamejiri wakati wa ugawaji wa vitendea kazi kwa wataalamu wa Ugani wa kilimo Wilaya ya Songea iliyofanyika tarehe 15 Septemba 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kuboresha utendaji kazi katika sekta ya Kilimo.
Ndile alisema “ni wajibu wa kila afisa kilimo kuhakikisha anasimamia shughuli za kilimo na kutoa ushauri kwa wakulima namna ya kulima kilimo chenye tija pamoja na kutambua aina ya udongo katika shamba lake, aina ya mazao yanayostahili kulimwa katika shamba lake, kupanda kwa wakati, kupalilia kwa wakati, pamoja na kuweka mbolea kwa wakati.”
Aliongeza kuwa, kilimo bora sio kulima eneo kubwa bali ni kuzingatia taratibu za kilimo pamoja na kutumia mbegu bora na ufuatiliaji na usimamizi bora wa kilimo.
Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa kwa wataalamu hao ni pamoja na, Kwa Manispaa ya Songea wamepkea Ganboot pair 28, Rain Coat 28, Pump Sprayer 28, Madaba wamepokea Soil Scanner 1, Printer 1, Desktop 1, Ganboot pair 17, Rain Coat 17, Pump Sprayer 17, Kishikwambi 1, pamoja na Lamination Machine 1, Kwa Halmashauri ya Wilaya wamepokea, Soil Scanner 1, Printer 1, Desktop 1, Ganboot pair 39, Rain Coat 39, Pump Sprayer 39, Kishikwambi 1 Lamination machine 1.
Akizungumza Afisa kilimo Manispaa ya Songea Zawadi Nguaro alitoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita kwa kuwawezesha vitendea kazi wataalamu wa idara ya kilimo ambapo wameahidi kufanya kazi kwa bidiii ili kufikia lengo la Serikali.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KIENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa