SEKTA ya Utalii katika mkoa wa Ruvuma inaendelea kufunguka baada ya kugundulika vivutio viwili vya utalii vilivyopo katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma.Vivutio hivyo ni bwawa ambalo linaitwa Beata lililopo kilometa nne toka katika Kijiji cha Ifinga .Kijiji cha Ifinga kipo umbali wa kilometa 48 toka barabara kuu ya Songea -Njombe.Paroko wa Parokia ya Ifinga Padre John Otete ameongoza hadi kilipo kivutio hicho ambacho kiligundulika na wamisionari wa kijerumani miaka ya 1930.Bwawa hilo ambalo lipo kati kati ya milima lina urefu wa meta zaidi ya 500.Maajabu ya bwawa hilo ni kwamba muda wote maji yake ni masafi na kuna samaki wengi ambao wamekuwa kivutio.
Kulingana na padre Otete,wajerumani baada ya kugundua bwawa hilo na namna lilivyowavutia waliamua kulipa jina la Beata kwa kilatini likiwa na maana ya utukufu.Bwawa hilo lilikuwa linatumika na wamisionari hao kwa kufanya pikiniki na kuogelea na walipoondoka wenyeji wa eneo hilo walikuwa wanaliogopo kulitumia wakiamini ni bwawa la mizimu na masheni.Hata hivyo baada ya Padre huyo kupelekwa katika eneo hilo tangu mwaka jana ameamua kuwaelimisha wananchi wa Ifinga kuwa bwawa hilo ni kivutio cha utalii wanatakiwa kulilinda kwa kutoharibu mazingira yake ambapo hivi sasa wananchi wanafurahia kivutio hicho ikiwa ni pamoja na kunywa maji yake ambayo yanaradha ya aina yake.
Tayari wataalam wa misitu TFS wamekwenda katika eneo la bwwwa hilo na kupima eneo hilo ambalo lipo ndani ya eneo la parokia ya Ifinga.Licha ya kivutio hicho kivutio kingine ambacho kinavutia wengi wanaosafri toka Lilondo kwenda Ifinga ni milima ya kupendeza ambayo Padre Otete anaifananisha na milima ya nchi ya Ujerumani na kusisitiza kuwa milima hiyo kipindi cha masikina inavuti wengi ambao wamekuwa wanasimama na kufanya utalii wa picha.
"Mimi nikifikahapa najiona kama nipo Ujerumani,kwa sababu milima hii inafanana na sana na ile ambayo niliiona nchini Ujerumani",anasisitiza padre Otete.
Makala imeandikwa na Albano Midelo simu 0784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa