MANISPAA ya Songea mkoani Ruvuma imeanza kutekeleza Mpango kabambe wa kutoa elimu kwa wafanyabiashara ili kusalimisha mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku kuanzia Juni Mosi mwaka huu.Katika siku ya kwanza ya kutekeleza mpango huu wafanyabiashara wanne katika Manispaa ya Songea wamesalimisha KG 1778 sawa na zaidi ya tani 1.7 za mifuko ya plastiki ambapo utekelezaji wa kuhakikisha mifuko yote ya rambo katika Manispaa ya Songea inatoweka itaendelea kufanywa kuanzia Juni 3 hadi Juni 14.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Pendo Ndumbaro ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati inayotekeleza agizo la marufuku ya kutumia mifuko ya rambo katika Manispaa ya Songea ametoa wito kwa wafanyabiashara ambao walikuwa wanauza mifuko ya rambo kutoa ushirikiano katika Kamati hiyo kuhakikisha kuwa mifuko yote wanaikabidhi katika kamati hiyo na kwamba kuendelea kutumia mifuko ya rambo ni kosa la Jinai ambapo mtuhumiwa akifikishwa Mahakamani anaweza kupata adhabu ya faini,kifungo au adhabu zote mbili.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa