TAASISI ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania ( TAFIRI) imetoa mafunzo ya utengenezaji wa chakula cha samaki kwa wafugaji 40 kutoka katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Mafunzo hayo yametolewa na Mtafiti Dr.Groria Yona kutoka TAFIRI Makao makuu jijini Dar es salaam pamoja na mambo mengine amesema mafunzo hayo yanaendelea kutolewa kwa muda wa siku mbili kuanzia 06/02/-07/02/2020 katika Ukumbi wa Songea Club kwa wafugaji wa Samaki Manispaa ya Songea.
Amelitaja Lengo kuu la kutolewa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Wafugaji wa Samaki namna ya kutengeneza malighafi za chakula cha Samaki ili waweze kupata Samaki wenye uzito stahiki kwa muda muafaka na kupata Samaki wenye thamani katika soko la Samaki.
“Mafunzo haya yanatolewa na TAFIRI katika mikoa saba(7) hapa nchini ambayo ni Ruvuma,Njombe,Geita,Dar es salaam,Morogoro,Pwani na Mwanza”,alisema Dr.Yona.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa