• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAGANGA wakuu wa Mikoa wapewa siku 30 kutathimini utendaji kazi wa Kamati za afya

Tarehe ya kuwekwa: May 6th, 2019

Waganga wakuu wa Mikoa Tanzania Bara wamepewa mwezi mmoja kuhakikisha kuwa wanazifanyia tathmini ya kina kamati za Uendeshaji Huduma za Afya za Mikoa na wilaya zao kuona kama zinaendana na kasi ya mabadiliko yanayokusudiwa na Serikali ya awamu ya tano.

Agizo hilo limetolewa jana mjini Songea na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt.Dorothy Gwajima wakati akizungumza  na wajumbe wa kamati ya Uendeshaji Huduma za Afya ya Mkoa wa Ruvuma pamoja za Halmashauri za wilaya ya  Namtumbo na Songea pamoja na Manispaa ya Songea.

Amesema anawapa siku 30 Waganga wakuu wa Mikoa yote kuhakikisha kuwa wanafanya tathmini ya wajumbe waliopo katika ofisi zao kama wanatosha kuendelea na nyadhifa zao za kusimamia jukumu la uendeshaji huduma za afya katika mikoa na halmashauri zao.

Dkt Gwajima ameongeza kuwa endapo itabainika kuwa baadhi ya wajumbe wa kamati hizo hawana sifa zinazowafanya kushindwa kutekeleza majukumu yao ya usimamizi na uendeshaji huduma za afya katika maeneo yao, waganga wakuu wa mikoa watalazimika kuwaweka pembeni wajumbe hao na kuunda upya kamati ambazo zitaweza kuiendeleza agenda ya mabadiliko katika sekta ya afya.

“Kinyume na hapo katika ziara hizi ninazoendelea kuzifanya mikoani nikikuta yupo Mganga Mkuu ambaye ametulia tu, mapungufu katika vituo bado yapo na amewezeshwa na serikali, ajue wazi kuwa wa kutokutosha wa kwanza atakuwa yeye,” amesema Dkt Gwajima na kuongeza:

“Haiwezekani tukute mapungufu madogo kabisa katika vituo, ambayo yangeweza kuonwa na wao walioko huko eti hayaonekani hadi tuje sisi kutoka Tamisemi ndiyo mapungufu hao yafanyiwe kazi,”amesisitiza Dkt Gwajima.

Naibu Katibu Mkuu huyo ameonya tabia iliyojengeka miongoni mwa wajumbe wa kamati za uendeshaji huduma ya afya kukimbilia kuomba msamaha pindi zinaposhindwa kutekeleza majukumu yake kwa makusudi.

Amesema huu ni wakati wa kuboresha sekta ya afya katika vituo vya afya na zahanati kwa kuhakikisha kuwa mazingira ya utoaji huduma yanaboreshwa ili yaweze kuwavutia wananchi wengi kukimbilia kupata huduma katika zahanati na vituo vya afya vinavyomilikiwa na serikali.

Dkt Gwajima amesema kuwa kamwe hatawapa nafasi wajumbe wa kamati za uendeshaji huduma za afya wa mikoa na wilaya ambao siku zote wamekuwa ni watu wa visingizio vya kuomba kusamehewa ama kupewa muda kuwa wamefahamu mapungufu yao.

Amesema angependa kuona kamati za uendeshaji huduma za afya katika  mikoa na halmashauri zikijikita katika kuongelea mambo makubwa yanayolenga kuishirikisha sekta na serikali kuu.

“Hivi vitu vidogo vidogo vya kitaalamu tubebe sisi wenyewe, wananchi wametuunga mkono, tumeweza kushirikiana nao kujenga zahanati na vituo vya afya katika mikoa na halmashauri zetu hivyo ni jukumu letu sasa kuhakikisha kuwa tunatoa huduma bora za afya kwa wananchi,” amesema.

Kwa mujibu wa Dkt.Gwajima, katika ziara zake alizokwisha zifanya katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Njombe na Ruvuma amejionea mapungufu mbalimbali ya utoaji wa huduma bora za afya katika vituo vya afya na zahanati.

Ameongeza kuwa mapungufu hayo ambayo ameyashuhudia kwenye vituo vya afya na zahanati zinazomilikiwa na umma yametokana na watendaji hao  kutopata usimamizi unaostahili kutoka kwa kamati za usimamizi  na uendeshaji wa huduma za afya za mikoa na halmashauri husika.

Dkt Gwajima anaamini kuwa kushindwa kwa kamati za uendeshaji ndiko kulikopelekea kukithiri kwa uchafu katika majengo ya vituo vya afya na zahanati nchini licha ya vituo hivyo kuwa na fedha za uendeshaji wake.

Sambamba na kuwataka waganga wakuu wa mikoa kuzitathmini kamati hizo, Dkt Gwajima amewataka waganga wakuu wote kutambua kuwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli ana agenda moja tu ya kuleta mabadiliko katika sekta ya afya.

 “Hatutapimwa kwa idadi ya semina au vituo vya afya tulivyojenga bali kwa ubora wa kazi za kuhudumia wananchi,” amesema.

Dkt Gwajima amebainisha mapungufu kadhaa aliyoyaona kwenye ziara yake kuwa ni pamoja kuwepo kwa malalamiko toka kwa wagonjwa na  kukosekana kwa takwimu sahihi za utendaji kazi

Akiwa katika kituo cha afya Mjimwema Manispaa ya Songea Naibu Katibu Mkuu Dkt.Gwajima alipokea kero za wagonjwa kuhusu uwepo wa kauli mbaya toka kwa wauguzi na tatizo la ukosefu dawa hususan  akina mama wajawazito

“Hapa Mjimwema nimebaini kasoro nyingi mojawapo kauli mbaya za watumishi na tatizo la dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa ” Dkt .Gwajima alionya.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Jairy Khanga ameahidi  kuchukua hatua za mapema kufanya mabadiliko ya utendaji kazi wa kamati za usimamizi wa huduma za afya katika mkoa wa Ruvuma .

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa