WAHASIBU katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wanapata mafunzo ya siku tatu ya Mfumo wa Maandalizi na Uwasilishaji wa Taarifa za Fedha(FFARS).Mafunzo hayo yanafanyika kwenye Ukumbi wa Manispaa ya Songea yakiwashirikisha wahasibu wa Makao makuu ya Manispaa ya Songea,vituo vya Afya,zahanati,shule za msingi na sekondari.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Christopher Ngonyani amesema mara baada ya mafunzo hayo,wahasibu waliopata mafunzo,watagawanywa katika zahanati,vituo vya Afya,shule za msingi na sekondari ili kusimamia mfumo wa FFARS.“Kila zahanati,vituo vya Afya,shule za msingi na sekondari inatakiwa kuandaa mpango na bajeti ya 2017/2018 kwa kutumia mfumo,wakishaandaa wanatakiwa kuzipeleka bajeti zao kwa wahasibu ili bajeti hizo ziingizwe kwenye mfumo wa FFARS’’,anasisitiza Ngonyani.
Ngonyani anasisitiza kuwa kuanzia mwaka wa fedha wa 2018/2019 shule za msingi na sekondari zilizosajiriwa zitaandaa bajeti zao moja kwa moja kulingana na mgawo wao wa fedha zinazotoka serikali kuu.
Taarifa imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa