Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, Wakili Bashir Muhoja, ametoa wito kwa watumishi wa Halmashauri kuzingatia mafunzo na maelekezo yanayotolewa kuhusu maandalizi ya Mpango Mkakati (SP), ambao ni nyenzo muhimu katika kupanga mwelekeo wa maendeleo ya miaka mitano ijayo.
Akizungumza katika kikao kazi cha maandalizi ya mipango na bajeti, Muhoja amesisitiza kuwa mpango mkakati ni dira na ramani ya maendeleo ya Manispaa, ikitoa mwongozo wa matumizi sahihi ya rasilimali ili kufikia malengo ya muda mrefu kwa ufanisi na uwajibikaji.
Mambo Mahususi Aliyosisitiza
Muhoja ameeleza kuwa bila mpango mkakati, bajeti huwa ya kubahatisha na mipango hukosa mwelekeo wa muda mrefu.
Mafunzo haya ya siku 3 (26–27 Novemba 2025) yanawahusisha wakuu wa idara, vitengo na watumishi wao, wakiwa wanajiandaa kutengeneza mpango mkakati wenye tija kwa Manispaa.
MWISHO.
Amina Pilly
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa