Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Manispaa ya Songea wametembelea banda la Manispaa hiyo katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale, Jijini Mbeya, tarehe 08 Agosti 2025.
Ziara hiyo imelenga kujionea ubunifu, mafanikio na teknolojia mbalimbali zinazowasilishwa na Manispaa ya Songea katika sekta ya kilimo, ufugaji, na maendeleo ya jamii. Pia, ilikuwa ni fursa ya kuhamasisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu baina ya wataalamu kutoka sekta mbalimbali.


Wakuu hao walipongeza juhudi zilizofanyika katika kuandaa na kuwasilisha shughuli za maendeleo zinazotekelezwa katika Manispaa hiyo, huku wakitoa wito kwa jamii kuendelea kushiriki kikamilifu katika maonesho hayo ya kilimo na mifugo.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa