WAKUU wa Idara na Vitengo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamepata mafunzo ya uandaaji wa taarifa kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji mapato yaliyofanyika kwa siku mbili kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa chini ya wakufunzi wake wametoa mafunzo ya uandaaji wa taarifa za CDR na CFR & LGRCIS ambao ni mfumo wa ukusanyaji mapato lengo likiwa ni kuhakikisha kila idara inajitengenezea bajeti na kufanya malipo mbalimbali.
Mkaguzi wa Ndani kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Adelin Komba amewasisitiza wakuu wa Idara na vitengo kuwa makini katika utumiaji wa mfumo huo ili kuweza kupata taarifa za bajeti zilizo sahihi na uhakika zaidi.
Kwa upande wake, Afisa TEHAMA wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mvano Mbalale ameeleza udhaifu wa mfumo huo na kuiomba serikali kuboresha baadhi ya programu ili kurahisisha utendaji wa kazi.
Naye, Afisa Biashara Manispaa ya Songea Furaha Joseph Mwangakala amesema kuwa mfumo una taarifa zisizo sahihi kutokana matumizi mabovu yaliyosababishwa na uelewa mdogo, pia ameomba watendaji wa TEHAMA wapunguziwe majukumu ikiwemo ulipaji wa leseni upitie moja kwa moja kwa Afisa Biashara ili kuepusha mwingiliano wa taarifa.
“Mfumo bado unahitaji marekebisho ili kuondoa taarifa chafu.” Amesema Mwakangala.
Mfumo wa ukusanyaji mapato ni miongoni mwa njia kuu ya kukuza uchumi wa Nchi ambapo mapato yanayokusanywa husaidia kuboresha shughuli mbalimabli za maendeleo na kuboresha mapato.
Imeandaliwa na
Bacilius Kumburu
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Agosti 26, 2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa