UDANGANYIFU KWENYE HALMASHARI UNAPOTEZA ASILIMIA TANO YA MAPATO KILA MWAKA
MHADHIRI wa Shule ya Biashara, Idara ya Fedha na Uhasibu Chuo Kikuu cha Mzumbe,Dk.Cosmas Mbogela anasema utafiti ambao ulifanywa na ACFE mwaka 2016, ulibaini kuwa vitendo vya udanganyifu katika Halmashauri na Taasisi nchini vinasababisha kila mwaka Halmashauri hizo kupoteza asilimia tano ya mapato yake yote.
Dk.Mbogela àmbaye anatoa mafunzo ya viashiria vya udanganyifu ( Fraud risks management ) na uandaaji wa Fraud Risks management policy, kwa wakuu wa Idara na Vitengo katika Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma, anabainisha kuwa kwa mujibu wa utafiti huo asilimia 71.4 ilitokana na udanganyifu wa ndani (internal perpetrators) na kwamba asilimia 16.6 ya udanganyifu huo katika Halmashauri ulibainika katika Idara ya Uhasibu na Fedha .
Katika hatua nyingine Dk Mbogela amewaambia wakuu wa Idara na Vitengo kuwa watumishi wa umma hawatakiwi kutumia Mali au vifaa vya serikali kwa shughuli zao binafsi. Ametolea mfano Mkuu wa Idara kutumia gari la serikali kwa shughuli zake binafsi ni udanganyifu na kwamba anafanya makosa kisheria.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa