Mkurugenzi Manispaa ya Songea Tina Sekambo akiwakilishwa na Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Songea bi Zakia Fandey, amewaasa walimu wote Manispaa ya Songea kufuata maelekezo yote yaliyotolewa na Serikali katika kupambana dhidi ya ugonjwa hatari wa CORONA katika maeneo ya kazi ili kudhibiti Maabukizi mapya ya Virus vya ugonjwa huo kwa Wanafunzi /Walimu wakiwa shuleni.
Bi Zakia ametamka hayo katika mafunzo ya kupambana dhidi ya ugonjwa hatari wa COVID-19, yaliyoshirikisha Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa shule sekondari, pamoja na Walimu wa kuu shule za Msingi yaliyofanyika kwa nyakati tofauti katika Ukumbi wa Manispaa ya Songea tarehe 22/06/2020.
Aidha, aliongeza kuwa” Katika kuendeleza jitihada za kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya Corona (COVID-19) Manispaa ya Songea imeandaa mkakati ambayo inalenga kuweka mazingira wezeshi ya udhibiti wa maambukizi ya COVID-19 katika Shule za Sekondari na Shule za Msingi. Pia alisema mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa ikiwa ni pamoja na kutakasa (Decontamination) mazingira yote ya shule, kutoa elimu kwa wanafunzi/ na walimu wote kuhusu ugonjwa wa COVID-19 pamoja na dalili zake na hatua za kuchukua ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo, Kuhakikisha uwepo wa vifaa vya kunawia mikono (sabuni na maji tiririka) kwa ajili ya usafi wa mikono katika kila eneo au maeneo ya madarasa, ofisi, kila geti/lango kuu, mabweni, maktaba, bwalo la chakula, vyoo na maeneo mengine muhimu, Pamoja na uwepo wa vifaa vya kunawa mikono vizingatie mahitaji ya eneo husika. Alisisitiza.”
Naye Afisa afya Manispaa ya Songea Maxensius Mahundi alisema Lengo la kutoa mafunzo haya ni kuwajengea uwezo katika kupambana na COVD-19 ambayo yatawasaidia kufahamu namna maambukizi yanavyoweza kutokea, dalili na jinsi ya kuchukua tahadhari.
Mahundi alisema Elimu iendelee kutolewa mara kwa mara kwa kupitia vikao vya kamati za Shule, Wananchi/Wazazi ili waweze kuhamasisha wanafunzi kuvaa barakoa wakati wanapokwenda au warudipo shuleni. Aliongeza kuwa wazazi/walezi wahimizwe kuwapatia watoto wao barakoa za vitambaa kabla ya kwenda shuleni.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KAIMU AFISA HABARI –MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa