Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne umeanza kufanyika leo nchi nzima huku kukiwa na jumla ya watahiniwa 485,866 waliosajiliwa kufanya mtihani huo kwa mwaka 2019 na kati yao wa shule ni 433,052 na 52,814 wa kujitegemea
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema kati ya watahiniwa hao wanaume ni 206,420 sawa na asilimia 47.67 na wanawake 226,632 sawa na asilimia 52.33 huku wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwa 842
Mwaka 2018 idadi ya watahiniwa wa shule waliosajiliwa walikuwa 427,181 na hivyo kuna ongezeko la jumla ya watahiniwa 5,871 kwa mwaka huu ukilinganisha na mwaka jana
Amewataka wasimamizi wa mitihani, wamiliki wa shule, walimu na wananchi kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu katika mtihani huu kwani Serikali haitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kujihusisha au kusababisha udanganyifu.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa