• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI Songea waaswa kupisha ujenzi barabara za Sovi na Majengo

Tarehe ya kuwekwa: May 24th, 2019

MKURUGENZI wa Manispaa ya Songea Tina Sekambo anatoa rai kwa wajasirimali wanaofanya biashara ndogo ndogo katika barabara ya Sovi hadi Planet Bar kuondoa bidhaa zao na vizuizi vingine ili kupisha utengenezaji wa barabara hiyo unaofanywa  na  Kampuni ya SIETICO inayojenga barabara za lami katika Mji wa Songea.

Kwa mujibu wa Sekambo,wajasirimali  wadogo wengine ambao wanatakiwa kuondoka ni wale wanaofanya biashara zao Kata ya Majengo katika barabara inayotoka katika  SACCOS ya Manispaa ya Songea kupitia shule ya Msingi Songea ambapo Kampuni ya SIETICO inatarajia kujenga mitaro ambayo inapita katika maeneo hayo na kuishia bonde la  Matomondo.

Ujenzi wa barabara kiwango cha lami km 8.6 katika barabara za katikati ya Mji ulianza kutekelezwa tarehe 01 Juni, 2015 na ulitarajia kukamilika tarehe 30 Juni, 2017 chini ya Mkandarasi M/s Lukolo Co Ltd.

Gharama ya mradi ilikuwa ni Tshs. 14,320,586,464.39 (pamoja na VAT). Mpaka kufikia tarehe 30 Juni, 2017 mkandarasi alilipwa kiasi cha Tshs. 2,204,887,742.00 mkandarasi alishindwa kukamilisha mradi kwa mujibu wa mkataba, hivyo Halmashauri ilisitisha mkataba wa Matengenezo ya Barabara.

kazi ya Ujenzi wa barabara km 10.3 kwa kiwango cha lami ilitangazwa tena mwezi Oktoba 2017 na kupatikana kwa mkandarasi M/S CHINA SICHUAN INTERNATIONAL CO-OPERATION CO. LTD.

Mradi huu umeanza kutekelezwa mwezi Machi, 2018 na unatarajiwa  kukamilika  Septemba, 2019. Mpaka sasa Mkandarasi ameshalipwa kiasi cha Tshs. 6,038,006,039.65 ikiwa ni malipo ya awali pamoja na kazi ambazo ameshafanya mpaka sasa hivi.

Hadi sasa Mradi huu umefikia asilimia 50 ya utekelezaji. Mradi huu baada ya kukamilika utagharimu kiasi cha Tshs. 13,104,078,000.20 ikiwa ni gharama alizolipwa mkandarasi wa awali pamoja na mkataba mpya unaoendelea.

Kukamilika kwa mradi huu kutarahisisha mawasiliano na  kuongeza fursa za ajira, kiuchumi na usafirishaji wa bidhaa na mazao.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Manispaa ya Songea 

Mei 23,2019

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa