Ujenzi wa barabara kiwango cha lami km 8.6 katika barabara za katikati ya Mji ulianza kutekelezwa tarehe 01 Juni, 2015 na ulitarajia kukamilika tarehe 30 Juni, 2017 chini ya Mkandarasi M/s Lukolo Co Ltd. Gharama ya mradi ilikuwa ni Tshs. 14,320,586,464.39 (pamoja na VAT). Mpaka kufikia tarehe 30 Juni, 2017 mkandarasi alilipwa kiasi cha Tshs. 2,204,887,742.00 mkandarasi alishindwa kukamilisha mradi kwa mujibu wa mkataba, hivyo Halmashauri ilisitisha mkataba wa Matengenezo ya Barabara.
kazi ya Ujenzi wa barabara km 10.3 kwa kiwango cha lami ilitangazwa tena mwezi Oktoba 2017 na kupatikana kwa mkandarasi M/S CHINA SICHUAN INTERNATIONAL CO-OPERATION CO. LTD. Mradi huu umeanza kutekelezwa mwezi Machi, 2018 na unategemewa kukamilika mwezi Septemba, 2019. Mpaka sasa Mkandarasi ameshalipwa kiasi cha Tshs. 6,038,006,039.65 ikiwa ni malipo ya awali pamoja na kazi ambazo ameshafanya mpaka sasa hivi. Mradi umefikia asilimia 45 ya utekelezaji. Mradi huu baada ya kukamilika utagharimu kiasi cha Tshs. 13,104,078,000.20 ikiwa ni gharama alizolipwa mkandarasai wa awali pamoja na mkataba mpya unaoendelea. Kukamilika kwa mradi huu utarahisisha mawasiliano, kuongeza fursa za kiuchumi na usafirishaji wa bidhaa na mazao.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa