SERIKALI wilayani Nkasi mkoani Rukwa imesema kuanzia sasa watakaotuhumiwa kuwapa mimba wanafunzi majina yao yatangazwa katika Redio ya Nkasi kila baada ya taarifa ya habari.
Mkuu wa wilaya ya Nkasi amesisitiza kuwa watuhumiwa hao picha zao na majina yao yatabandikwa kwenye mbao za matangazo pia watasakwa kila mahali na kufikishwa kwenye vyombo vya dola lengo likiwa ni kukomesha mimba za utotoni kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme pia ametangaza vita kali dhidi ya wanaume ambao wanawapa mimba wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
Mkakati anaoutumia hivi sasa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ni ule unaojulikana kama magauni manne ambayo ni mtoto wa kike kuwa ndani ya sare ya shule, gauni la pili ni la kuhitimu masomo,gauni la tatu ni la harusi na gauni la nne ni la kuvaa wakati wa ujauzito ambapo mtoto wa kike aatakuwa ametimiza ndoto zake.
Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wasichana 8000 kila mwaka huacha shule kutokana na ujauzito Kati yao 3,000 ni wanafunzi wa shule za msingi na wanafunzi zadi ya 5000 wa shule za sekondari.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa