Jimbo la Songea lina vituo vya kupigia kura 500 na jumla ya wasimamizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi 1,542 wamepata mafunzo ya kusimamia vituo vya uchaguzi ambayo yameanza kutolewa leo tarehe 26 hadi 27 oktoba 2025 kuelekea siku ya uchaguzi.
Akizungumza Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Songea Mjini Alto Liwolelu amesema " uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu za kikatiba na sheria ambazo hupaswa kufuatwa na kuzingatiwa katika ngazi ya vituo ambapo mchakato na matokeo ya uchaguzi kwa kila kiti cha Rais, Ubunge na udiwani ndio yanapoanzia. Amewataka wasimamizi kufuata taratibu zote zilizowekwa ili uchaguzi uwe huru na haki.
Mafunzo hayo yametolewa katika kumbi mbalimbali katika Jimbo la Somgea mjini.
Mwisho.
Kitengo cha mawasiliano Serikalini
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa