UCHAGUZI mdogo wa ubunge Jimbo la Songea mjini unatarajia kufanyika Januari 13 Kama ulivyopangwa na Tume ya Uchaguzi .
Halmashauri ya Manispaa ya Songea tayari imeteua orodha ya majina 321 ya wasimamizi wa vituo na wasaidizi wao ambao wanapata mafunzo katika kumbi mbalimbali ukiwemo ukumbi huu wa Manispaa ya Songea.
Mafunzo yamefunguliwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Tina Sekambo ambaye pamoja na mambo mengine amewaasa wasimamizi kuwa makini kuangalia majina sahihi ya wapiga kura,kujiepusha na udanganyifu wowote ambao unaweza kusababisha kupelekwa mahakamani.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa