WATENDAJI 116 kutoka katika Halmashauri za Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamepewa mafunzo ya utunzaji wa kumbukumbu za fedha na usimamizi wa fedha za serikali za mitaa.Mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea,yamewashirikisha watendaji wa Mtaa 95,watendaji wa Kata 21 na wataalam wa Manispaa.
Mgeni rasmi katika mafunzo hayo alikuwa ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Alhaj Abdul Hassan Mshaweji ambaye alisisitiza watendaji wa mitaa kuibua vyanzo vipya katika mitaa na kata zao ili kusaidia kuongeza mapato ya Halmashauri ambayo hivi sasa yamefikia asilimia 85.Mada zilizofundishwa ni taratibu za usimamizi wa fedha,uandaaji wa malipo,utunzajii wa kumbukumbu za fedha na taratibu za manunuzi.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa