WATENDAJI wa kata na Mitaa wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamesainishwa mkataba wa afua za lishe Mkoani Ruvuma
Afisa Lishe wa Manispaa ya Songea Anna Nombo akizungumza katika mkutano huo na watendaji wa kata amewataka kuwajibika katika kutekeleza malengo yote yaliyoko katika mkataba huo ili kuweza kupunguza utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano, wanawake wajawazito na akina mama wanaonyonyesha kwa kuwa hali ya utapiamlo katika Mkoa ni kubwa zaidi.
Nombo, amesema kuwa utafiti wa afaya na Demogarfia ya mwaka 2015 na 2016 unaonesha kuwa udumavu umefikia asilimia 44 ambao unasabababishwa na mambo mbalimbali kama vile ulishaji duni,maradhi ya mara kwa mara na huduma hafifu za malezi na makuzi ya awali kwa watoto wadogo.
“Hivyo ili kufanikisha haya yote kunahitajika usimamizi wa hali ya juu kujenga taifa bora,Ni vyema tukashirikiana ili kutetea na kulinda maisha ya ndugu zetu.” Amesema Nombo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa ya Manispaa ya Songea ambaye ni Mtendaji wa Kata ya Ndilimalitembo Bakari Kawina amewasisitiza watendaji wote kushirkiana kwa pamoja ili kufanikisha dhamira kuu iliyoko ndani ya mkataba huo na amewahasa kwa yeyote atakayekiuka atachukuliwa hatua za kisheria..
Pia amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa viongozi kwa kuwa yote yaliyoainishwa katika mkataba yanawalenga wao na taifa kwa ujumla.
Mkataba huu utakuwa wa muda wa miaka mitatu na utaanza tarehe 01 julai, 2019 hadi tarehe 30 juni, 2021 ambapo Mkataba huu utapimwa kila baada ya miezi 6 ya utekelezaji.
Imeandaliwa na
Bacilius Kumburu
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
22 August, 2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa