MGANGA Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Dkt.Mameritha Basike amesema wateja 100 wapya wamegundulika kuwa na maambukiz mapya ya virusi vya UKIMWI mjini Songea.Akizungumza ofisini kwake Dkt Basike amesema idadi hiyo imebainika katika kipindi cha Januari hadi Agosti 2019 jumla ya watu 2527 walipima afya zao, kati yao wateja 100 waligundulika kuwa na VVU sawa na asilimia 3.95.
Ameitaja zahanati ya Bombambili ni moja ya zahanti zinazotoa huduma za mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI, Huduma hizi zilianza mwaka 2004. ambapo Huduma ya kutokomeza maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto, inatolewa kwa akina baba, mama wajawazito, wanaonyonyesha na kwa watoto.
Amesema Kwa kipindi cha Januari hadi Agosti 2019 jumla ya kina mama wajawazito na anaonyonyesha 493 walipima VVU, kati yao 18 waligundulika kuwa na VVU sawa na asilimia 3.64. Hadi sasa kituo kina idadi ya kinamama wajawazito na wanaonyonyesha 80 wanaotumia dawa za kufubaza VVU.
Aidha watoto 45 waliozaliwa na kina mama wenye VVU kwa kipindi cha Januari hadi Agosti 2019, walichukuliwa sampuli za damu na kufanyiwa uchunguzi, kati yao watoto 2 waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU sawa na asilimia 4.49.
Amesema kutokana na kuboresha mazingira kuwa mazuri ya utoaji wa huduma, imepelekea ongezeko la wateja waliosajiriwa na kuanza dawa kutoka wateja 179 kwa kipindi cha Januari – Disemba 2018 hadi kufikia wateja 188 kwa kipindi cha Januari hadi Agosti 2019. na kwamba kwa kipindi cha Julai 2018hadi Juni 2019, zahanati imepokea dawa za kufubaza makali yavirusi vya UKIMWI zenye thamani ya Tshs. 11,289,851.49 kutoka Bohari ya Dawa Iringa.
Imeandikwa na Farida Musa
wa Kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Septemba 26,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa