HALI ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma bado inatishia ustawi wa jamii ya kuongezeka maambukizi ya ugonjwa huo Takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha Maambukizi katika kipindi cha mwaka 2017 ni 3.1 ambapo watu waliopima walikuwa 88,255 kati yao wanawake 48,185 na wanaume 40,070.
Kulingana na takwimu hizo kati ya waliopima, Waliogundulika kuwa na Virusi vya UKIMWI walikuwa 2,780 kati yao wanawake walikuwa 1,729 na Wanaume 1,051. Halmashauri ya Manispaa ya Songea ina vituo 26 vinavyotoa huduma za CTC ambavyo vimesajiliwa na jumla ya wagonjwa 25,619 kati yao 12,349 wameanzishiwa dawa za ARV’s.
Hata hivyo katika kukabiliana na maambukizi mapya,Halmashauri ya Manispaa ya Songea inaendelea kutoa mafunzo ya UKIMWI mahali pa kazi, kutoa mafunzo kwa jamii kupitia klabu za vijana na kutumia vikundi vya waathirika na kutoa ushuhuda katika mikutano ya jamii.
Wananchi wote waliopo kwenye dawa za kufubaza virusi vya ukimwi,wanahimizwa kujua wingi wa virusi kwenye damu zao na kutoa elimu kupitia sinema pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya kuhusu kujikinga dhidi ya maambukizi ya UKIMWI.
Uchunguzi umebaini kuwa Mwitikio wa Jamii katika suala zima la kudhibiti UKIMWI ni mkubwa. Hii inatokana na Takwimu zilizopo katika Manispaa ya Songea.Takwimu zinaonesha kuwa watu 10,097 katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea wanaugua UKIMWI na wapo kwenye dawa hadi sasa ambapo Zaidi ya watu 23,000 katika Manispaa hiyo wanaishi na virusi vya UKIMWI.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Juni 18,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa