WATUMISHI WA MANISPAA YA SONGEA ,WAANZA MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA BAJETI
WATUMISHI 49 katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wanapata mafunzo ya siku tano ya Mfumo wa kieletroniki ambayo yatapunguza gharama za uendeshaji za maandalizi,uwasilishaji na utekelezaji wa mipango ya bajeti mpya.
Mafunzo hayo yamefunguliwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Eng.Samwel Sanya katika Ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Mchumi Christopher Ngonyani amesema mfumo huo mpya ambao umeanza kutumika rasmi hapa nchini kuanzia mwezi huu Septemba,utapunguza gharama za safari kwa wakuu wa Idara na wahasibu katika Halmashauri nchini kote ambapo sasa kupitia mfumo mpya kila kitu katika mchakato wa Bajeti kitafanyika katika Halmashauri kwa njia ya Mfumo wa kieletroniki hivyo safari zitapunguzwa na kuondolewa.
Kwa mujibu wa Ngonyani,Baada ya mafunzo haya wakuu wa Idara,Vitengo na watumishi wengine katika Halmashauri wataanza kuandaa bajeti ya mwaka 2018/2019 kupitia katika mfumo huu mpya ambapo utekelezaji wa maandalizi ya bajeti hiyo mpya unatarajia kuanza Oktoba 2017.
Mfumo huo mpya umezinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mwezi huu Makao makuu ya nchi mjini Dodoma na mfumo huo mpya unatarajiwa kutumika katika Halmashauri zote nchini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa