Katika kufanikisha usimamizi wa utendaji kazi katika utumishi wa umma kila mtumishi wa umma alikuwa anapimwa utendaji wake wa kazi kwa kutumia mfumo wa siri uliojulikana kama ‘‘Taarifa ya Siri ya Utendaji Kazi ya Mtumishi wa Serikali’’(Confidential Appraisal System).
Ambapo Kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2023, utendaji kazi wa Watumishi wa Umma umekuwa ukipimwa kwa kutumia Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (Open Performance Review and Appraisal System - OPRAS), pia kuanzia Mwaka 2018 hadi 2023, kwa upande wa taasisi, ilikuwa na Mfumo wa mikataba ya Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma (Institutional Performance Contracting System (IPCS).
Aidha, 2023 na kuendelea, utendaji kazi wa mtumishi wa umma na utendaji kazi wa taasisi ya umma utasimamiwa na Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma ambao una sehemu mbili ambazo ni Public Employees Performance Management Information System (PEPMIS) ambao ni sehemu ya kwanza ya Mfumo Mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi ambao unachukua nafasi ya OPRAS, na Public Institutions Performance Management Information System (PIPMIS) ni sehemu ya pili ya Mfumo Mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi ambao unachukua nafasi ya IPCS katika kupima utendaji kazi wa Taasisi ya Umma.
Hayo yamejiri wakati wa mafunzo ya Mfumo wa thamani ya mahitaji ya Rasilimali watu Mkoani Ruvuma inayofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kuanzia 20Novemba hadi 24 Novemba 2023 ambayo yamehudhuriwa na wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa lengo la Kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa na taasisi nyingine katika Mkoa kufanya Tathmini ya Rasilimali watu katika Mkoa na kubaini Mahitaji ya Rasilimali watu.
Akizungumza Mkurugenzi Maendeleo ya Sera Ofisi ya Rais Menejiment na Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Cyrus Kapinga alisema “Mfumo wa Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu uliokuwa unatumika kwa muda mrefu katika Taasisi za Umma ulikuwa ni wa kutumia Job List Forms ambapo ulikuwa unatumia vigezo mbalimbali katika kubaini mahitaji ya watumishi ikiwemo, Muundo na Mgawanyo wa Mahitaji, Sheria na Miongozo mbalimbali iliyopo, na kazi zinazofanyika kwa mzunguko yaani shift.”
Mfumo huo wa kuandaa mahitaji kwa kutumia Joblist Forms umekuwa na changamoto kutokana na kutumia zaidi njia ya majadiliano na hivyo kusababisha maamuzi ya idadi ya watumishi wanaohitajika kutegemea zaidi utashi wa mwenye Taasisi na Mwezeshaji, ambapo licha ya kutumika kwa Mfumo huo bado kumekuwepo na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na Malalamiko ya waajiri kuhusu upungufu/uhaba wa watumishi, Kukosekana kwa takwimu sahihi zinazoongoza Waajiri katika kuandaa maombi ya ajira mpya, Kukosekana takwimu sahihi zinazoongoza OR MUUUB kutoa vibali vya ajira, na takwimu za mahitaji ya watumishi yanayoandaliwa na Waajiri kuwekwa katika Mfumo wa taarifa za Watumishi na Mishahara (HCMIS) kutokuwa halisia.
Hata hivyo, Ili kuondokana na changamoto hizo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ilichukua hatua ya ujenzi wa Mfumo wa Tathmini ya Rasilimaliwatu (HR Assessment System) ambao ni Mfumo wa kisayansi unakokotoa mahitaji ya watumishi kwa kufanya uchambuzi wa uzito wa majukumu (Work Load Analysis), pia unawewezesha kubaini mahitaji ya Kada ya Walimu nchi nzima kwa kutumia njia ya uwiano na Mahitaji ya Maafisa, Maafisa wasaidizi, pamoja na Viongozi na kada saidizi kwa kutumia fomu maalum katika mfumo. Bw. Kapinga “alibainisha”.
Amewataka watumishi wote kutenga muda kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo na kutoa ushirikiano wa pamoja na kuwa tayari kupata mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma (PEPMIS/PIPMIS) na Mfumo wa HR Assessment pamoja na kutekeleza majukumu watakayopewa na wataalam wa Mifumo ya PEPMIS/PIPMIS na HR Assessment.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa