HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imetoa mafunzo maalum kwa watumishi wake yanayohusiana na masuala ya kinidhamu yaliyofanyika kwa siku mbili kwenye ukumbi wa manispaa hiyo mjini Songea.Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Mkuu wa Idara ya Utumishi Lewis Mnyambwa amesema Manispaa imeandaa mafunzo hayo kwa wakuu wa Idara na Vitengo na kwamba lengo ni kuwajengea uwezo wa kiutendaji wakuu hao namna ya kushughulikia masuala ya kinidhamu ya watumishi wa umma ili kuboresha utendaji na usimamizi wa rasilimali watu katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa