Tanzania huungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya wazee Duniani, kwa ustawi wa wazee ambayo hauadhimishwa kila ifikapo tarehe 01 oktoba ya kila mwaka ambapo siku hii ilitengwa na baraza la Umoja wa mataifa kupitia azimio namba 45/106 la mwaka 1990.
Kauli hiyo imetolewa jana katika maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani iliyofanyika katika uwanja wa Majimaji Manispaa ya Songea wenye lengo kuu la Kuelimisha na Kujenga hamasa na uelewa katika kuboresha upatikanaji wa huduma na haki za wazee katika Jamii.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ambaye aliwakilishwa na Afisa Ustawi wa jamii Mkoa wa Ruvuma Victor Nyenza ambapo alianza kwa kutembelea vibanda vya maonesho mbalimbali pamoja na vibanda vya upimaji wa afya.
Nyenza aliwapongeza wazee hao kwa kushiriki maadhimisho siku ya wazee duniani kwa kupima afya zao ambapo wazee waliojitokeza kupima uzito na sukari walikuwa 37 kati ya hao (me 25, na ke 12), waliopima vvu ni 67 kati ya hao (me 38 ) na (ke 29).
Awali katika taarifa iliyosomwa na Wazee wa baraza hilo ambayo ilisema nanukuu “tunakuomba utufikishie shukrani zetu za dhati kwa Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Joseph Pombe Magufuli kwa kuifikisha nchi yetu hapa tulipo katika awamu yake ya kwanza ya miaka mitano kwa kushugulikia masuala yanayowahusu wazee pamoja kuwawezesha watoto wetu toka ngazi ya shule za awali hadi sekondari kupata elimu bure, pamoja na Kuwepo kwa wizara maalumu inayosghulikia masuala ya wazee. “ mwisho wa kunukuu.
Wakizitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili wazee hao ni kukosa fursa ya kupata mikopo kama inavyotolewa kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu, pamoja na kutokuwepo kwa baraza huru la wazee ngazi ya mkoa,
Nyenza akitolea majibu kwa baadhi ya changamoto zilizotajwa na wazee hao ambapo aliahidi kuzichukua na kuzipeleka ofisi husika kwa ajili ya kuzishughulikia mapema iwezekanavyo.
Alibainisha kuwa kila mmoja wetu anawajibu wa kuwatunza wazee ili waweze kuwa azina ya baadaye na kujenga kizazi chenye uzalendo ambacho kitarithi desturi ya kuwapenda na kuwatunza wazee.
Kauli mbiu ya mwaka huu 2020 “Familia na Jamii tuwajibike kuwatunza wazee’’
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
02 octoba 2020
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa