Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) inaendelea kutoa mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura yanayoendelea kufanyika katika kumbi tofauti Manispaa ya Songea na yanatarajia kukamilika hapo kesho tarehe 26 oktoba mwaka huu.
Lengo la mafunzo hayo kwa wasimamizi wasaidizi wa vituo ni kutoa mwongozo na utaratibu wa kuzingatia wakati wa kuandaa kituo, kufungua kituo, kupiga kura, kuhesabu kura, na kufunga kituo.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Songea mjini Tina Sekambo amesema “ ni muhimu wasimamizi na wasaidizi wa vituo kuhakikisha kuwepo kwa utulivu na usalama katika kituo cha kupigia kura, akiyataja mafanikio ya uchaguzi yatatokana utekelezaji wa majukumu yako kwa kufanya kazi kwa weledi, uadilifu, kwa kuzingatia miongozo na maelekezo yanayotolewa na tume ili kuzuwia kusababisha vurugu, na malalamiko.” Tina amesisitiza.
Tina alibainisha kuwa uchaguzi ni hatua na hutekelezwa kwa kufuata sheia hivyo aliwaasa wasimamizi wote wa vituo wasifanye kazi kwa mazoea kwasababu kila hatua ya uchaguzi ni maelekezo ya sheria sio maamuzi ya mtu binafsi.
Alisema Jimbo la Songea Mjini lina vituo 393 na kwa kila kituo kitakuwa na msimamizi wa kituo na wasaidizi wake ili kuweza kusimamia uchaguzi vizuri kama maelekezo ya Tume yalivyoelekeza.
Aliwaaasa wasimamizi wa vituo na wasaidizi wake kuandaa kituo mapema iwezekanavyo na kuhakikisha kinafunguliwa saa 1:00 asubuhi ikiwa pamoja na kuweka kituturi sehemu salama ili mpiga kura aweze kupiga kura kwa uhuru na haki.
Naye Afisa wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Agatha Nchimbi amesema “ Tume imejipanga vizuri katika kuhakikisha zoezi hili linakwenda vizuri na vifaa vyote vya vinavyopaswa kuwepo kwenye kituo cha kupigia kura vinakuwepo, hata hivyo wasimamizi wote wanapaswa kuzingatia vipaumbele kwa wazee, walemavu, wagonjwa, wajawazito, na wanaonyonyesha.
Nao washiriki wa mafunzo hayo kwa nyakati tofauti walisema wamepokea mafunzo hayo na wameahidi kufuata maelekezo yote ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kufanikisha zoezi zima la uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika juma lijalo 28 oktoba mwaka huu.
MTAYARISHAJI;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
25 oktoba 20
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa