Mbunge wa jimbo la Nyasa Mhandisi stella Manyanya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji amemkabidhi baiskeli yaenye thamani ya Tsh1,500,000/=( milioni moja laki tano) mlemavu wa miguu ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa alipofanya ziara katika Kijiji cha malini kata ya Mtipwili Hivi karibuni Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.
Baiskeli hiyo imekabidhiwa na Katibu wa Mbunge Manyanya ndugu Cosmas Nyoni Nyumbani kwa John Mapunda ambaye ni mwenye ulemavu anayeishi katika kijiji cha Malini Kata ya Mtipwili Wilayani Wilaya ya Nyasa ili kumrahishisa mwenye ulemvu huyo wa viungo.
Manyanya alifafanua kuwa kwa kushirikiana na mwanae anayeitwa Hope exaveria ambaye pia ni mwenyeulemavu aliamumua kumsaidia baiskeli hiyo mwenye ulemavu huyo kwa kuwa akiwa katika ziara yake alipokuwa kijiji cha Malimi alipokea ombi la Mwenye ulemavu huyo kuomba Baiskeli kwa kuwa alikuwa anapata shida ya kutembea na kubadilishana mawazo na wenzake hivyo baiskeli itamsaidia kutembea na kubadilishana mawazo na na ndugu wenzie.
Aliongeza kuwa anatambua ulemavu kwa kuwa ana mtoto ambaye ni mwenye ulemavu na anaona walemavu nao ni binadamu kama walivyo binadamu wengine ambao wanahitaji upendo na kuthaminiwa ikiwa ni pamoja na kusaidiwa au kutatuliwa changamoto zao.
“Nimetumwa na Mbunge Stella Manyanya ili nikuletee baiskeli ambayo ulimuomba akiwa katika ziara katika kijiji hiki cha Malini kama tunavomfahamu Mbunge wetu kila anachoahidi anakitekeleza na leo hii amekuletea kwa kushirikiana na mwanae anayeitw Hope Exaveria ambaye naye ni mlemavu wamekubaliana kukusaidia wewe ili uweze kutembea vizuri na kubadilishana na mawazo na marafiki zako na ndugu jamaa na marafiki”alisema Katibu huyo wa Mbunge.
Akipokea msaada huo ndugu John Mapunda alimshukuru sana Mbunge na kusema kuwa kabla ya kupata baiskeli hiyo alikuwa anapata shida ya kutembea kwa kuwa alikuwa anatembea kwa kutambaa kwa shida lakini mara baada ya kupata baiskeli hiyo atapata fursa ya kuwatembelea ndugu jamaa na marafiki na wakati mwingine atakuwa akibadilishana mawazo na rafiki zake kijiweni.
Mh Manyanya amekuwa na kawaida ya kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum na hivi karibuni akiwa katika ziara ya siku nane katika Tarafa ya Mpepo Katika Kijiji cha Lunyele Katika shule ya msingi Lunyele aliwasaidia ushauri wa matibabu kwa watoto watatu waliozaliwa katika familia tatu tofauti na kumwagiza Mganga mkuu wa Wilaya ya Nyasa Dkt Aroin Hyera kwenda kuwapa ushauri wa kitaalam watoto watatu ambao walizaliwa wakiwa na vichwa vikubwa wazazi wao wakiwa hawajui cha kufanya.
Naye mwenyekiti wa kijiji cha malini Kata ya Mtipwili alimshukuru sana kwa kuwajali na kuwasaidi wananchi wake wenye mahitaji maalum na kumwomba aendelee na moyo huo huo anao hawatamwangusha kwa kuyasema kwa wananchi miradi yote anayotekeleza kwa Wananchi.
IMETOLEWA NA
NETHO C.SICHALI
AFISA HABARI
WILAYA YA NYASA
0783662568
TAR.02/11/2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa