WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewaagiza watumishi wa umma katika Halmashauri zote nchini kuwahudumia wananchi kwa wakati na kuacha tabia ya kuwasumbua kwamba wafike kesho kupata huduma.
Akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Namtumbo katika siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi katika mkoa wa Ruvuma Waziri Mkuu amesisitiza kuwa serikali haitaki kuona wananchi wanazagaa nje katika Halmashauri kwa kusubiri huduma na kwamba mtumishi ambaye atashindwa kutoa huduma kwa wananchi wanyonge ataondolewa kwa sababu serikali inataka wananchi wanyonge wapate huduma katika Halmashauri kwa wakati bila usumbufu.
Waziri Mkuu yupo mkoani Ruvuma katika ziara ya siku tatu ambapo anafanya ziara katika wilaya za Namtumbo na Tunduru.Katika ziara hiyo Waziri Mkuu anafungua miradi,kuzungumza na watumishi wa umma na kufanya mikutano ya hadhara na wananchi.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa