Na
Amina pilly
20 Agosti 2022
Waziri wa katiba na sheria Dkt. Damasi Ndumbaro amewataka wananchi wote wa Songea mjini kujitokeza katika zoezi la sensa itakayofanyika tarehe 23 agosti 2022.
Hayo yametamkwa jana tarehe 20 agosti 2022 katika uwanja wa majimaji iliyoshirikisha wananchi mbalimbali, wadau wa michezo, viongozi wa vyama vya siasa kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujitokeza katika zoezi la sensa.
Dkt. Ndumbaro amesema kuwa sensa inaiwezesha serikali kupata takwimu sahihi zitakazo saidia katika upangaji wa mipango ya maendeleo ya mji wa songea na taifa kwa ujumla, ambapo alisema kuwa “sensa ni ajenda yetu kwa mwaka huu ambayo itawezesha kupata takwimu ya ongezeko la watu ambapo itasaidia kupandisha hadhi ya mji kutoka Manispaa na kwenda kuwa jiji”.
Alisema makarani wote watakaohusika katika zoezi la sensa wahakikishe wanatekeleza wajibu wao kwa kuzingatia mafunzo waliyopewa ili kufanikisha ukusanyaji wa takwimu sahihi unafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Aliongeza kuwa michezo ni muhimu na inasaidia kujenga afya ya mwili hivyo amewataka wananchi kuendelea kufanya mazoezi kwa kila mwisho wa mwezi ambapo amewaondoa shaka wanamichezo wa timu mbalimbali zinazoshiriki mazoezi ambapo ameahidi kuwa mlezi wa timu hizo kwa kusaidia vitu muhimu kama jezi, mpira na t-shirt kwa lengo la kuwaunga mkono SOMI FOUNDATION 2022 SENSA MARATHON ambayo ni imeanzishwa na jamii ya Songea kwa madhumuni ya kudumisha michezo na mazoezi ya viungo vya mwili na shughuli nyinginezo za kijamii.
Aidha Dkt. Ndumbaro ( MB) ametoa T-shirt kwa SOMI FOUNDATION na washiriki wote waliohudhuria kwenye mazoezi, Mipira Miwili kwa timu za Mpira wa Miguu na kikapu pamoja na Medali kwa wanamazoezi hao.
Naye mbunge wa viti maalumu Ruvuma Mhe. Mariamu Nyoka, amewarai wananchi kujitoa katika zoezi la sensa na kutoa taarifa sahihi ili kufanikisha Serikali kupata takwimu sahihi ambazo zitasaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Ruvuma na taifa kwa ujumla.
Mheshimiwa Mariamu (MB) alisema katika kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Mbunge Dkt. Ndumbaro ametoa zawadi mbalimbali zinazohusisha vifaa vya michezo kwa dhumuni la kuhamasisha wananchi kushiriki katika michezo, na kuwahamasisha kujitokeza katika zoezi la sense ambapo miongoni mwa zawadi zilizotolewa ni pamoja na bibs seti mbili, jezi seti mbili, mpira wa basketball mmoja na mipira ya netball miwili za timu mbili za wanawake, pamoja na mipira ya miguu miwili na jezi za timu mbili za wanaume.
Wananchi nao kwa wakati tofauti, wamewapongeza waheshimiwa wabunge hao kwa kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ambayo imehusisha uhamasishaji wa Sensa kwa wananchi kujitokeze kuhesabiwa tarehe 23 agosti 2022 ambapo kwa umoja wao wameahidi kujitokeza kuhesabiwa.
MWISHO
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa