• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAZIRI wa Kilimo aiagiza NFRA kuweka mikakati ya kununua mahindi

Tarehe ya kuwekwa: January 7th, 2019

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) pamoja na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko zimetakiwa kuandaa mikakati ya haraka kuanisha jinsi watakavyo nunua mazao ya wakulima nchini.

Wakati NFRA imetakiwa kuainisha namna ya kununua nafaka za wakulima kwa upande wa Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko yenyewe imetakiwa kujikita katika ununuzi wa mazao mbalimbali ya wakulima ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko ya mazao ndani na nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 5 Januari 2019 na Mhe Japhet Hasunga (Mb) Waziri wa Kilimo, wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa.

Alisema kuwa Wizara yake imekuwa ikihamasisha wakulima nchini kuzalisha kwa wingi mazao kwa ajili ya chakula na biashara lakini inapofika hatua ya kuuza bei zinakuwa ndogo jambo ambalo serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli haitalifumbia macho kamwe.

Pamoja na mambo mengine waziri Hasunga ameupongeza Uongozi wa wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA kwa ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa (Silos) katika maeneo nane ya kanda saba za wakala ambapo ujenzi huo utaongeza uwezo wa kuhifadhi mahindi kutoka Tani251,000 za sasa hadi Tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.

Mradi huo wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi umeanza kujengwa katika Manispaa ya Songea (Ruvuma), Dodoma, Mpanda (Katavi), Makambako (Njombe), Mbozi (Songwe), Sumbawanga (Rukwa), Shinyanga Mjini (Shinyanga), na Babati (Manyara) ambapo Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland zilisaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu Septemba 2015 wa Dola milioni 55 sawa na sh. bilioni 124, kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo, ambao utaongeza uwezo wa hifadhi ya chakula.

Mhe Hasunga amesema kuwa pundi utakapokamilika ujenzi wa maghala na vihenge hivyo utapunguza gharama mbalimbali zilizokuwa zinatumika kwa ajili ya kununua madawa ya kufukiza mahindi sambamba na gharama za kununua magunia ya kuhifadhia mahindi.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amemtaka Kaimu Mtendaji Mkuu wa wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba kuweka msisitizo zaidi wa kununua nafaka ya mahindi kwani katika kipindi chake serikali haitotoa hela kwa ajili ya ununuzi wa mahindi badala yake NFRA ijipange kibiashara ili iweze kununua nafaka nyingi na kujiendesha.

Alisema kuwa huu sio muda wa NFRA kusubiri kupewa mtaji na serikali badala yake kufikiria tofauti na kuanza kufanya biashara ili kufikia walau ununuzi wa nafaka kwa Tani zaidi ya 300,000.

Vilevile, ameutaka Wakala wa majengo Tanzania (TBA) kusimamia kwa weledi mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa ili kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati ili kuwanufaisha wananchi.

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa